PARIS SAINT GERMAIN YA UFARANSA YAMNASA ANGEL DI MARIA KUTOKA MACHESTER UNITED.
Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain PSG hii leo wamethibitisha kukamilisha usajili wa winga raia wa Argentina Angel Di Maria .
Klabu hiyo ya Ufaransa imekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 45 kwa klabu yake ya zamani Manchester United kiasi ambacho ni hasara ya paundi milioni 10.
United ilimnunua Di Maria kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 55 na kumfanya kuwa mchezaji ghali kuliko wote kwenye historia ya ligi ya England .
Di Maria anaondoka United akiwa amecheza kwa msimu mmoja pekee akiwa amesajiliwa toka klabu ya Real Madrid.
Winga huyo ametia saini mkataba wa miaka minne ambao utamuweka ndani ya klabu hiyo ya Ufaransa hadi mwaka 2019 .
Kwa Hisani ya Mtandao
No comments: