LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA NNE: UGONJWA WA KISUKARI UNAVYOATHIRI JAMII.

Soma HAPA Sehemu ya Tatu ili Twende Sawa.
Upo umuhimu wa kupima kisukari mapema basi, ili kuepuka mtu kuishi nacho kwa muda mrefu pasipo kujua, na kusababisha madhara kusambaa mwilini na kumwathiri mwathirika. 
Ni muhimu kuzingatia mazoezi, uzito, lishe na ushauri wa wataalamu wa afya, kwa sababu husaidia kupunguza makali na madhara yatokanayo na kisukari. 

Mgonjwa anaweza kuzuia madhara yatokanayo na kisukari kwa kuzingatia maelekezo, masharti na ushauri wa wahudumu wa afya, hasa kuhusu chakula na mazoezi na maelekezo ya utumiaji sahihi wa dawa au insulin. 

Mgonjwa hatakiwi kuvuta sigara, awe anapima kiwango chake cha shinikizo la damu mara kwa mara na kuhakikisha kiwango chake cha lehemu kipo katika uwiano unaotakiwa.

maelekezo yahusuyo njia na jinsi ya kupima na kujua kiwango cha kawaida cha sukari mwilini.

Kujitambua wakati kiwango cha sukari kikiwa juu kupindukia ni kwa kupima damu angalau mara tatu kwa siku, ikiwa ni pamoja na kabla ya kwenda kulala. Mara nyingi watu hupima asubuhi au alfajiri wanapoamka, mchana wa adhuhuri au alasiri na jioni au usiku kabla ya kulala. 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii  Steven Kebwe  (pichani) akitoa tamko  la serikali mwaka 2014 kuhusu ugonjwa wa kisukari jinsi unavyo athiri watu nchini.
Dk Kebwe anasema  gharama za kutibu mgonjwa mmoja wa kisukari kwa mwaka hapa nchini ni sh.408,000 na utafiti wa mwaka 2012uliofanywa  katika wilaya 50 nchini ulionyesha asilimia 9.1 ya watu huugua ugonjwa huo bila wenyewe kujua.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Naibu Waziri wa Afya Kebwe Stephen wakati akitoa tamko la serikali kuhusu siku ya ugonjwa huo ambayo huadhimishwa kila mwaka duniani kote, anasema ugonjwa huo umekuwa na changamoto kubwa kwa vile husababishwa na ulaji usiofaa.
Anasema takwimu zinaonesha watoto wanaokabiliwa na ugonjwa wa kisukari mwaka huu 2014 ni kati ya asilimia 15 hadi 20 ya wagonjwa wote kisukari wanaotibiwa kwenye kliniki mbalimbali nchini.
Dk.Kebwe anasema watu wengine wanakuwa na dalili lakini huwa hawachukui hatua za mapema ili kuweza kuzuia ugonjwa huo kuendelea ambao dalili zake ni rahisi kuzitambua nazo ni kusikia njaa kila wakati,kukojoa mara kwa mara,kupungua uzito, na mwili kukosa nguvu. 

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani mwaka 2014 ni "Ulaji unaofaa, huanza na mlo wa asubuhi" ililenga kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya ulaji unaofaa ili kuepuka matatizo mbalimbali yanayotokana na ugonjwa wa kisukari katika jamii. 

Hata hivyo kutokana na wananchi wengi wa Tanzania wanakipatao cha chini hivyo ni jukumu la Serikali,wadau,Taasisi mbalimbali  pamoja na jamii kwa ujumla kuwasaidia wagonjwa wakisukari kuwapatia mashine za kupimia jambo litakalosaidia kuwapa unafuu katika suala zima la kupima na kujua hali yake kiafya.
                MWISHO
Imeandaliwa na Judith Ferdinand  0757804962 Kwa msaada wa mtandao na mashirika ya habari.

No comments:

Powered by Blogger.