LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA: NIFANYE NINI ILI NIWE NA AFYA BORA (SOUND PHYSICAL HEALTH).

Afya ni kitu cha msingi sana kwa binadamu, kama afya yako isipokuwa njema basi hutoweza kufanya jambo lolote lile iwe ni uzalishaji,kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kusimamia miradi yako n.k. Kuna msemo unaosema Afya ni mtaji namba moja hii ni kweli kabisa.
Kuwa na afya bora inamaanisha kwamba akili na mwili wako vinafanya kazi kwa amani/maelewano. Watu wengi wakiwa wanaongelea afya huwa wanaiongelea katika mwili tuu lakini maana halisi ya kuwa na afya ni kuwepo kwa uelewano mzuri kati ya akili yako na mwili vyote kwa pamoja viweze kufanya kazi vema. Na unatakiwa kujua kwamba Afya ya akili na Afya ya mwili vinategemeana. Mwili ukikosa lishe bora hata namna mtu anavyofikiri inadhoofika.Kwa hiyo ni lazima kuzingatia kutunza Afya zetu.
Afya ya akili inamaanisha mtu anajua ni nini anachosikiliza, anachojifunza na mtazamo ambao anaokuwa nao. Tumejifunza sana katika mada zilizopita kwamba mtu anapokuwa na mtazamo hasi anauwezekano mkubwa wa kupatwa na magonjwa ya vidonda vya tumbo, msongo wa mawazo n.k
Mambo ya kuzingatia katika kujenga afya ya akili ni pamoja na...... 1.Kujiwekea utaratibu wa kujisomea mambo mapya kila siku japo kwa dk 30 au zaidi ili kupanua fikra na mawazo yako.
Lakini kuwa makini na hakikisha kwamba hicho unachokisoma ni cha kujenga akili yako ,vitu ambavyo unaangalia pia vina uwezo mkubwa wa kuathiri akili yako hivyo angalia tuu vitu ambavyo vinakujenga kiakili ,marafiki ambao unakaa nao na stori au habari mbalimbali unazozisikia kwa watu maana kuna uwezekano mkubwa wa kuathiri afya ya akili yako.
2.Kujiwekea utaratibu wa kuhudhuria semina mbalimbali za ujasiriamali au dini ili kukuimarisha katika kazi au biashara fulani ambayo unayoifanya na kujiweka karibu na Muumba wako.
3.Kuweka utaratibu kila siku wa kusoma Qurani takatifu au Biblia takatifu ili kujiimarisha kiimani na mahusiano yako na Mungu yaimarike.
Afya ya mwili inamaanisha mtu anajua ni nini ambacho anakula katika mlo wake na anapata faida gani katika kile anachokula,epuka kula kula ovyo vitu usivyojua vina msaada gani mwilini mwako.
Je umeshawahi kujiuliza ni kwa nini kadiri watu wanavyopata fedha nyingi ndivyo wanavyozidi kusumbuliwa na magonjwa mengi ikiwemo presha, kisukari,kiribatumbo n.k ? Ni kwa sababu huwa wanakulakula ovyo pasipo kujua ni nini wanachokula hivyo hujikuta hela wanazozipata wanazitumia kwa kiasi kikubwa hospitalini.
Mambo ya kuzingatia ili kuweza kulinda afya mwili wako ni pamoja na haya...
1.Kuwa na tabia ya kula mlo kamili kila siku ili uweze kupata virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika mwilini ukiwa na tabia ya kupata viritubisho viwili tuu kwa mfano wanga na protini upo katika hatari ya kunenepa na kuongezeka sana uzito na hii itasababisha matatizo mwilini mwako.
2.Jijengee utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuchangamsha viungo vya mwili wako, mwili wa binadamu unahitaji mazoezi na haya yanasaidia sana kuwezesha viungo kufanya kazi salama hivyo hata damu itaweza kupita katika mishipa ya ateri,veini na kapilari vizuri.
3.Lakini pia jali mwili wako kwa kuvaa vizuri na pindi unapokuwa mazingira ya baridi hakikisha unavaa nguo za kotoni ili kuweza kutengeneza joto la kutosha mwilini.
4.Usijihusishe na matumizi ya pombe na sigara maana yana athari kubwa katika mwili wako na hali hii inaweza ikaathiri mishipa yako ya damu hivyo ukapatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
5.Ushijihusishe na mapenzi kabla ya wakati kuwa makini sana kama hujaowa au kuolewa ni vema ukasubiria mpaka wakati ukafika kuna wale wanaoshindwa kufanya ivi basi hakikisha unatumia kinga siku hizi kuna magonjwa mengi sana ikiwepo ukimwi kiwa makini sana katika hili.
6.Kuwa na utamaduni wa kupima afya yako mara kwa mara hii itakusaidia kujua kama una tatizo na kulitatua tatizo mapema kabla halijawa kubwa.
7.Epuka na kaa mbali na matumizi ya dawa za kulevya maana zina mdhara katika mwili na akili yako kwa ujumla.
Ukiwa na afya bora itakuwezesha wewe kufanya mambo yako kwa nguvu na pasipo matatizo ya aina yoyote, mtu hajafanikiwa kama anasumbuliwa na magonjwa kama presha,kisukari, lehemu n.k, mtu aliefanikiwa kifedha lakini bado anasumbuliwa na afya bado huyo hajafanikiwa kufanikiwa ni katika kila eneo yaani , Afya, fedha, mahusiano, imani, n.k
SHEA NA WENZAKO WENGI SANA KAMA KWELI UNAJALI AFYA ZAO NA UNAWAPENDA. LIFE SECRETS COMPANY. SIKU NJEMA.
email us: allnhump@gmail.com

No comments:

Powered by Blogger.