WANAHABARI NCHINI WAASWA NAMNA YA KUANDIKA NA KURIPOTI HABARI ZA UCHAGUZI.
Mmoja wa Wakufunzi katika Semina kwa Waandishi wa Habari juu ya kuripoti habari za Uchaguzi Kanda ya Ziwa ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mitandao ya Jamii Forums pamoja na Fikra Pevu, Maxence Melo akiwasilisha Mada juu ya Uharifu wa Mitandaoni na Sheria za Takwimu.
Na:George GB PazzoWaandishi wa Habari nchini wameaswa kuripoti matukio pamoja na habari sahihi katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu, zikiwa zimelenga kuwa na manufaa katika taifa na siyo kuibua migogoro.
Rai hiyo ilitolewa jana Jijini Mwanza katika Semina kwa Waandishi wa Habari kutoka Kanda ya Ziwa, iliyolenga kuwajengea Uwezo wa namna ya kuripoti Habari za Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu nchini.
Wakufunzi Katika Semna hiyo, waliwahimiza wanahabari kuandika habari kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na kuepuka kuandika habari zenye mrengo mmoja jambo ambalo linaweza kuibua migogoro miongoni mwa wagombea na wapiga kura.
Semina hiyo iliandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania MISATAN kwa kushirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda na inatarajia kufikia tamati hii leo.
No comments: