LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA NNE YA MAKALA IITWAYO "NIA".

Bonyeza HAPA Ili Usome Sehemu ya Tatu na Twende Sawa.
SABABU ZINGINE ZA KUAMSHA NIA NDANI MWAKO.
Kunywa maji mengi ya kutosha asubuhi na wakati wa mchana, mwili unapokosa maji kwa mda mrefu mtu huwa anajisikia kuchoka hata kama anakuwa anakula vizuri na kulala kwa wakati jitahidi kila siku unywe maji glasi nane mpaka kumi na mbili yaani lita 2.5 mpaka 3 za maji. Hii itakupa nguvu na NIA ya kufanya mambo yako kila siku.
Kuwa ni mtu wa kujichanganya na watu wengine lakini wale ambao mnafanana kimtazamo. Usije ukawa chanya na ukatumia siku yako nzima kukaa na watu hasi wanaolaumu serikali na ndugu zao, ambao hawataki kuchukua jukumu la maisha yao kwa asilimia wenyewe kwa asilimia 100, wanaofikiri hatima ya maisha yao iko kwa mtu mwingine sio wao wenyewe lakini pia kama una mambo ya kujadili usipendelee kujadilia nyumbani nenda mbali na nyumbani .
Pendelea kufanya mazoezi wakati wa asubuhi, mazoezi ya asubuhi yanakupa ari na nguvu ya kukabiliana na siku nzima yanaandaa mwili na akili yako kwa ajili ya siku nyingine mpya. Ni muhimu ukajua kwamba mazoezi sio kwa ajili ya kuwasha NIA tuu ni kwa ajili ya mwili na akili yako, viungo vya mwili wako ili vifanye kazi vizuri vinahitaji mazoezi hii itawezesha damu ipite kwenye mishipa vizuri na usipokuwa una utaratibu wa kufanya mazoezi na ukawa huli mlo kamili basi lazima utanenepa tuu hilo halina ubishi.
Panga angalau kufanya kitu kimoja kila siku ambacho kinakupa raha pindi ukiwa unakifanya na kinakufanya ufikiri zaidi hii itasisimua NIA yako juu ya hicho kitu na mambo mengine ambayo utayafanya katika siku hiyo. Kwa mfano unaweza ukawa ni mfanya biashara lakini pia unapenda sana kuandika stori au pengine kuandika makala za kuelimisha jamii yako, sasa baada ya kutoka kwenye biashara yako ukaoga vizuri basi pata matunda yako na maji au chai ya mchaichai mezani hakikisha mazingira yanakuwa tulivu kisha uanze kuandika kama ni stori au makala yaaani chochote kile unachopenda kukifanya.
Pata muda wa kutosha kupumzika na ratiba yako ya kulala isiwe inabadilika badilika kuwa na ratiba inayoeleweka kama ni saa nne kamili ndio unalala basi ikifika saa nne hakikisha upo kitandani. Jua katika siku kuna masaa 24 yaani 8 ya kufanya kazi, 8 ya kufanya mambo binafsi, 8 ya kulala.Mtu mzima unatakiwa kulala masaa saba mpaka nane kila siku acha tabia ya kujinyima usingizi unajizeesha na utachoka kabla ya muda wako, jua kwamba usipolala vya kutosha NIA yako hudumaa ndio ile unaelezea mtu kitu huku unasinzia au unapiga miayo.
Punguza matumizi ya kafeini, sigara na pombe kwa mfano punguza matumizi ya chai ya kahawa, kahawa husisimua mwili pale unapoinywa lakini huwa haiwezi kukupa nguvu ya kuendelea na huo msisimko mpaka jioni badala yake tumia Chai ya mchaichai kwa sababu inaimarisha kinga na kumbukumbu lakini pia humpa mtu nguvu ya kutosha kupambana siku nzima.
Kuwa na tabia ya kujipongeza, hapa namaanisha pale unapofanya kitu kizuri kikafanikiwa basi usiache kujipongeza kwa kwenda sehemu fulani nzuri au kununua kitu fulani ulichokuwa unakipenda na hakikisha wakati unafanya hivyo unapiga picha za kutosha hii itazidi kuchochea NIA iliyopo ndani yako zaidi na zaidi na hata kipindi ukiwa chini unaweza kutumia tena picha hizi hizi kujiinua na ukawa juu kwa kujikumbushia.Mwalimu wangu Jihm Rohn alikiwa akisema mara kadhaa kwamba picha ya kitu imebeba maneno 1000 na hii ni kweli kabisa kwa sababu binadamu anafikiri kwa picha.
Usinywe wala usile lisaa limoja kabla ya kulala kwa sababu ukifanya hivyo utausababisha mwili wako ufanye kazi ya ziada na ya kutumia nguvu zaidi ili uweze kumeng'enya chakula hicho kitu ambacho kinaweza kikasababisha usilale vizuri saa zingine, na unywaji wa pombe usiku husababisha mtu kuamka amka usiku hivyo huwa anajipunja usingizi hakikisha unamaliza mambo yako ya unywaji saa moja jioni ili kama unalala saa nne uwe tayari umeshakojoa vya kutosha. Na pindi unapoamka amka asubuhi kunywa maji ya moto glasi mbili yenye limao au ndimu hii itakusaidia kuondoa sumu zilizobakia tumboni baada ya mmeng'enyo wa chakula lakini pia ni njia nzuri ya kuchoma mafuta yanayokuwa mwilini kwa watu ambao ni wanene kupindukia. MWISHO
Imeandaliwa na; Life Secrets Company 
PHONE:0689 452/670 /0765 536 842 EMAIL: allnhumph@ gmail.com

No comments:

Powered by Blogger.