LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YAKIRI KUWA MAJI YA MGODI WA ACACIA YALIOINGIA KIJIJINI KAKOLA MWEZI JANUARI YALIKUWA NA SUMU.

Na:Shaban Njia
Serikali kupitia Baraza la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) imesema kuwa maji yaliyomiminika kutoka katika moja ya  Mabwawa ya maji ya Sumu katika Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu na kuingia katika kijiji cha Namba tisa kilichopo Kata ya Kokala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga mwezi januari mwaka huu yalikuwa na sumu.

Akiongea kwa niaba ya NEMC Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya, alisema kuwa baada ya maji hayo kupasua kingo za moja ya Mabwawa yanayohifadhi maji yenye sumu kali aina ya synide na kuingia katika kijiji hicho yalisababisha uharibifu mkubwa ikiwemo uharibifu wa mazao, vyanzo vya maji pamoja na mifugo kuathirika.

Kufuatia tukio hilo Serikali ya Wilaya ya Kahama kupitia kwa Mkuu huyo wa wilaya ilisitisha shughuli za Kilimo pamoja kuzuia Wananchi wa Kijiji hicho kutumia maji ya Visima hadi Baraza la hifadhi ya mazingira nchini litakapotoa majibu baada ya kufanya uchunguzi.

Aliendelea kusema  kuwa baada ya NEMC kufanya uchunguzi ilibainika kuwa sumu iliymwagika katika Kijiji hicho ilikuwa na kiwango cha 1.126 PPM kiwango ambacho ni kikubwa na kuitaka Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi huo wa Bulyanhulu kuhakikisha kuwa inawafidia Wananchi wa Maeneo yaliyoathirika kutokana na kushindwa kujishughulisha na shughuli za uzalishaji ikiwemo Kilimo

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa kiwango cha  sumu cha kawaida kinatakiwa kuwa 0.001PPM na kuongeza kuwa kutokana na NEMC kugundua kuwa maji yale yalikuwa na sumu ni vyema Kampuni ya Acacia ikawafidia Wananchi maeneo mengine waondoke katika maeneo yaliyoathirika ili Kampuni hiyo iweze kuendelea na shughuli zake za uchimbaji kwa wananchi hao wako karibu na eneo la mgodi.

Wakiongea na Waandishi wa Habari, Wananchi wa Kijiji hicho walisema kuwa kutoka na sumu hiyo kuingia katika mashamba yao wanaiomba Serikali kuhakikisha kuwa wanalipwa fidia zao kwani kwa kipindi kirefu wamekaa bila ya kufanya shughuli zozote za kimaendeleo hali iliyowaathiri kiuchumi.

No comments:

Powered by Blogger.