SEHEMU YA PILI: UGONJWA WA KISUKARI UNAVYOATHIRI JAMII.
Soma HAPA Sehemu ya Kwanza Ili Twende Sawa.
Kundi la pili ni wagonjwa ni ambao kongosho lao
haliwezi kutoa kichocheo cha Insulini kabisa. Hwa ni lazima watumie tiba na
dawa(sindano za Insulin) ili kuwezesha sukari inayopatikana kwenye damu kuingia
katika viungo vya mwili kama ini na misuli, hivyo wanatakiwa kuchoma sindano
kabla ya kula kulingana na aina ya insulini aliyonayo mgonjwa.
Pia anasema dawa ya Insulini imegawanyika
katika makundi matatu ambayo ni ;
Insulini ya maji yenye ufito wa
rangi ya njano,ambayo inaanza kufanya kazi baada ya dakika 30,na inadumu kwa
masaa 4 hadi 6.
Insulini ya maziwa yenye ufito wa rangi ya
kijani hufanya kazi baada ya masaa 2,inadumu kwa muda wa masaa12 hadi 16.
Insulini ya mchanganyiko yenye ufito wa rangi ya
brauni,hufanya kazi baada yadakika 30,inadumu kwa masaa 12 hadi 16.
Pia sindano hizo uchomwa sehemu za
bega ,tumbo,makalio, begani a tumbo ni pale unapochomwa na mtu, dawa
hizo zinatakiwa kuhifadhiwa katika jokofu,mtungi au kopo la mkaa.
Anasema viashiria vinavyoweza kupelekea
kuugua ugonjwa wa Kisukari ni kiriba tumbo,unene
uliopitiliza, historia ya kisukari kwenye ukoo,baadhi ya
madawa yanasababishaugonjwa huo,msongo wa mawazo, umri zaidi ya miaka
40, kutojishughulisha, kutokufanya mazoezi ipasavyo.
Pia wakinanamama wanajifungua watoto wenye
uzito mkubwa zaidi ya kilo 4,maradhi yatokanayo na kuharibika
kongosho,tezi ya shingo,wakina mama wenye historia ya kuwa na kisukari wakati
wa ujauzito,wako katika kundi hatarishi la kupata kisukari hapo baadae pamoja
na watumiaji wa pombe na sigara.
Mhana anazitaja dalili za mtu kujua kuwa ana
ugonjwa wa Kisukari kuwa ni pamoja na;
Kiu ya mara kwa mara na unywaji wa maji mengi
ata kama ni wakati wa baridi,kukojoa mara kwa mara mkojo mwingi,kupungua uzito
bila ya sababu maalumu ata kama unakula vizuri, kizunguzungu, kutoona vizuri au
kupungua kwa uwezo wa kuona.
Nakauongeza kuwa dalili za sukari
kupungua mwili kwa mtu ambaye nimuathirika wa ugonjwa wa kisukari tayari
ni,kumwa na njaa sana,kuwa na hasira ata kwa kitu kisichoeleweka,mwili kukosa
nguvu,kupungua uwezo wa kufikiri,jasho jembamba,mapigo ya
moyo kwenda haraka haraka,kuumwa kichwa ,kutetemeka,na kichefuchefu.
Na kwa baadae kama hajapatiwa tiba mapema
atatokwa na jasho jingina mwili kuwa wa baridi,kupelekea hadi kupoteza
fahamu,degedege na wakati mwingine kufunga kauli au kupoteza maisha.
Pia Mhana anaelezea madharayatokanayo na
ugonjwa wa kisukari kuwa ni pamoja na kupatwa na kiharusi, kupooza na kupoteza
fahamu(kumbukumbu), upungufu wa kuona ,mtoto wa jicho,magonjwa ya kinywa na
kung’oka meno,shinikizo la damu,mshtuko wa moyo na kushindwa kufanya kazi,kupungua
kwa nguvu za kiume hatimaye kukosa kabisa,ganzi katika mwilividonda na hatimaye
kukatwa viungo vya mwili hasa miguu na vidple vyake.
Anaelezea mambo 5 ambayo mgonjwa wa kisukari
anatakiwa kuzingatia na kuyafuata ili kumfanya aishi maisha marefu.
Mosi ni Usafi wa Kinywa na Meno;mgonjwa wa kisukari
anatakiwa kupiga mswaki angalau mara Mbili ni kwa siku,ikibidi kila baada ya mloili
kuondoa mabaki ya chakula kinywani yanayoweza kusababisha kutengeneza bacteria
watakaoshambulia kinywa.
Tatu ni Kutumia mswaki bora,ili kuepuka madhara
yatokanayo na michubuko kwenye fizi.Dawa ya meno ni nzuri lakini inapokosekana
basi mgonjwa anashauriwa kutumia jivu la mkaa au chumvi.
Nne Mgonjwa wa kisukari anashauriwa kumuona
daktari au wataalamu wa magonjwa ya kinywa na meno angalau mara moja kwa mwaka
kwa wale wasiokuwa na tatizo, ila kwa wenye matatizo ya fizi na kutoboka kwa
meno wamuone daktali mara 1hadi 3 kwa mwaka kulingana na uwezo wa mtu.
Na tano ni Utunzaji wa miguu ambapo ugonjwa wa kisukari huleta
madhara ya miguu kwa kuathiri mishipa ya fahamu na mzunguko wa damu,matokeo
yake mgonjwa huanza kuhisi ganzi,hivyo anatakiwa kutunza miguu ili kupunguza
ukatwaji viungo hasa miguu.
Hata hivyo mgonjwa anapaswa kuhakikisha kuwa miguu yake anaisfisha
vizuri kisha kuikausha mara baada ya kusafisha kwa kutumia taulo au
kitaambaalaini na safihasa katikati ya vidole ,pia anapaswa kuikagua kila
mara/siku.
Apake mafuta ili kuzuia mipasuko ya ngozi, kama
ni mnene sana hawezi kuinama, inatakiwa aombe msaada wa ndugu aliye karibu, pia
anatakiwa kuvaa viatu muda wote ndani na nje ya nyumba ili kuepusha kuchomwa na
vitu vyenye ncha kali na kusababisha kidonda ambacho ni Atari kwa mwili wake.
Pia anapaswa kusafisha mwili mara kwa mara,pia
awe na uwezo wa kugundua tatizo mapema katiksa mguu wake kama kidonda
,lengelenge,kubadilika kwa rangi kwenye mguu uvimbe au mchubuko wowote,ili
akapatiwe matibabu haraka kabla ya tatizo kuwa kubwa.
Utunzaji wa kucha; Mgonjwa wa kisukari
anatakiwa asiwe na kucha ndefu,kwani anaweza kujichubua nazo wakati wa kutembea
au vinginevyo na kusababisha kidonda ambacho kitapelekea kukatwa kwa
viungo mwili kama mguu.
Itaendelea, Imeandaliwa na Judith Ferdinand; 0757804962 Kwa msaada wa mtandao na mashirika ya habari.
No comments: