LIVE STREAM ADS

Header Ads

SOMA KILICHOELEZWA NA MWAKILISHI WA KAMPUNI YA GESI YA ORYX KATIKA MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA.

Judith Ferdinand na Neema Emmanuel
Jamii imeshauriwa kutumia nishati ya gesi katika matumizi mbalimbali kwa kuwa ina gharama nafuu na husaidia katika kutunza mazingira jambo linalosaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mwakilishi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Kanda ya Ziwa Tumain Nestory wakati akizungumza na Binagi Media Group katika Maonyesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenae yanayofanyika kwa Kanda ya Ziwa katika Viwanja vya Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Nestory alisema kuwa jamii ikitumia nishati ya gesi katika matumizi mbalimbali hususani ya upishi, itasaidia kutunza mazingira kwa kuacha kukata miti ovyo kwa ajili matumizi ya kuni na mkaa.

“utumiaji wa nishati ya gesi katika matumizi mbalimbali hasa ya upishi yatatusaidia kukabiliana na uharibifu wa mazingira, kwani tutaacha shughuli za ukataji miti ovyo kwa ajili ya kupata kuni na mkaa, hivyo tutapa hewa safi pamoja na kuepukana na magonjwa ya milipuko yanayokana na uharibifu huo”. Alisema Nestory.

Pia alisema faida nyingine itokanayo na utumijaji wa gesi, ni kuokoa muda kwani urahisisha kupika, gharama zake ni nafuu ukilinganisha na nishati zingine kama mkaa na kuni.

Hata hivyo aliiomba serikali kupunguza kodi  za uingizwaji wa gesi nchini, ili wananchi wa kipato cha chini Waweze kumudu gharama za matumizi ya gesi.

Aidha aliwaomba waingizaji na wauzaji wa nishati ya gesi kupunguza gharama za uzaaji ili kusaidia kukidhi mahitaji hata kwa wananchi wenye hali duni ya kipato.

Kauli mbiu ya Oryx katika maonyesho ya nanenane mwaka huu ni  “Matokeo makubwa sasa, Tuchague viongozi bora kwa kilimo na ufugaji, pika, tunza mazingira na gesi,”.

No comments:

Powered by Blogger.