SEHEMU YA TATU: UGONJWA WA KISUKARI UNAVYOATHIRI JAMII.
Soma HAPA Sehemu ya Pili ili Twende Sawa.
Mgonjwa pia anatakiwa atumie kitu kisichokuwa
na ncha kali mfano mashine ya kukatia kucha,na kama anatatizo la kutoona
hapatiwe msaada.
Pia akate kucha kwa kufata mzunguko ili asije
kuacha ncha ,ambayu inaweza kumchoma au kumkata na kumsababishia kidonda.
Uvaaji wa viatu; Mgonjwa wa kisukari anatakiwa
kuzingatia kuvaa viatu muda wote,pia kutovaa viatu na soksi zinazo bana ili
kuepuka kuathiri mzunguko wa damu,mishipa ya fahamu,michubuko ya
ngozi,malengelenge na hatimaye kusababisha vidonda.
Pia mgonjwa anatakiwa kuchunguza viatu kabla
ya kuvaa ,ili kujua kama kuna msumari au wadudu watakaoweza kusababisha kumdhru
na kupelekea kupata kidonda.
Viatu ndani viwe vilaini na kwenye kisigino
nje vigumu ili kusaidia kuzuia vitu vyenye ncha kali kama msumari,vipande vya
chupa kutomdhuru vilevile view vyenye visigino vifupi.
Moto; mgonjwa wa kisukari anatakiwa kutopenda
kuota moto,naikitokea ameota anatakiwa kuchukuliwa tahadhari ili asiweze
kuungua na kusababisha jeraha ambalo ni hatari kutokana na hali yake.
Wakati wa kupika anatakiwa asitumie kitaambaa
kushikia sufuria au chungu na badala yake atumie mbanio,baada ya kupika ni
vyema kuzima moto kwa maji ya baridi,ili kuepuka kukanyaga na kuungua.
Pia kama anatumia maji ya moto kuoga inabidi
atumie kiwiko kupima kama yanafaa ili kuepuka mchubuko.
Mhana anaeleza kuwa mgonjwa wakisukari
anatakiwa kula chakula kwa kuzingaria mlo kamili ambao unamakundi matano ya
chakula kama.
Kundi la kwanza la Vyakula vya
nafaka, mzizi na ndizi, mgonjwa anatakiwa kutumia aina ya chakula hiki kwa
kiwango kidogo, ambacho ni sawa na ngumi yake, ila visiwe vimekobolewa.
“Vyakula vya nafaka ni kama mahindi, ngano, mchele,
ulezi, mtama, uwele. Vyakula vya mzizi viazi mviringo, magimbi, viazi vikuu, mihogo,
viazi vitamu.
Aina ya ndizi zote,lakini mgonjwa anapaswa
kula kiasi ili asisababishe,kushiba sana na kupelekea sukari kupanda”. Anasema
Mhana.
Kundi la pili ni vyakula jamii ya kunde na
asili ya wanyama; Anasema jamii ya kunde ni maharage, kunde, njugumawe, mbaazi,
njegere, choroko, karanga, dengu na fiwi, nazinatakiwa kula kiasi chja ngumi.
Vyakula vyenye asili ya wanyama ni aina zote
za nyamaambayo mgon jwa anapaswa kula nusu kilo kwa wiki,maziwa kunywa kila
siku nusu lita, samaki, jibini, dagaa, mayai matatu kwa wiki, pamoja na wadudu
wanaoliwa kama kumbikumbi na senene.
Kundi la tatu ni mbogamboga; Hizi hujumuisha
zile za majani yanayoliwa kama majani ya maboga, kunde, maharage, tembele, mchicha,
sukuma wiki, spinachi, bamia, karoti, matango, figili na nyingine nyingi, katika
kundi hili mgonjwa anatakiwa kutumia kwa wingi kulingana na uwezo wake.
Kundi la nne ni Mtunda; Mgonjwa wa kisukari
anatakiwa kula matunda kwa kiasi
kidogo ila kila siku, maembe,mananasi, ubuyu,machungwa,
mapera, zambarau na mengine mengi.
Nakuongeza kuwa mgonjwa wa kisukari anatakiwa
kupendelea kula matunda zaidi kulikuyatengenezea juisi jambo linasabaisha
kupunguza virutubisho vinavypatikana kwenye matunda, pia atakiwi kula muwa.
Kundi la tano ni mafuta na sukari;mgonjwa wa
kisukari anatakiwa kutumia mafuta ya kupikia yatokane na mimea na siyo wanyama
(mbegu zitoazo mafuta kama ufuta, korosho, kweme, alizeti na karanga, kwa kiasi
kidogo), pia asitumie sukari ya aina yoyote.
Hata hivyo anasema kuwa mgonjwa wa kisukari
anatakiwa kupunguza ulaji wa chumvi, mafuta na sukari, pia wasipende kutumia
vitu vya kiwandani.
Vilevile anaeleza kuwa mgonjwa wa
kisukari anatakiwa kuzingatia kupta milo 6,kwa sikuambayo 3kamili na mingine 3
midogo.
Mhana anasema mgonjwqa wa kisukari anapaswa
asubuhi apate chai ya maziwa, uji wa lishe au mahindi ambayo hayajakobolewa, lakini
visiwe na sukari pamoja na vipande viwili vya mkate.
Saa nne asubuhi kula kidogo, tunda kama embe
au chungwa moja, kikombe cha uji na kadhalika. Saa 7 mchana kula chakula kamili
kama ugali, wali, viazi hku ukiweka kiasi kikubwa cha mbogamboga, bila kusahau
tunda kama papai, parachichi robo kipande pamoja na ndizi mbivu moja.
Saa kumi jioni kula kidogo
kama chai au maziwa kikombe kimoja na kitafunwa chochote lakini
kisiwe na sukari,saa kumi na mbili jioni unakula kachumbali, mbogamboga na
matunda kama chungwa 1.
Pia muda wa saa 2 au 3 unakula mlo
kamili kama wali, ugali, ndizi kwa kuzingatia usawa wa ngumi huku ukiweka
mboghamboga kwa wingi na amatunda.
Pamoja na kuzingatia mlo hulaji huo mgonjwa
wakisukari anapaswa kunywa maji kwa kiwango kikubwa ili kusaidia mzunguko wa
damu na kupunguza sukari mwilini.
Mhana anasema kuwa mazoezi kwa mgonjwa wa
kisukari ni muhimu, hivyo anatakiwa kuruka kamba , kucheza mziki, mpira,
jogging kwa nusu saa angalau mara nne hadi tano kwa wiki na unatakiwa ufanye
ukiwa na ndugu au rafiki, kisha tembea na kitambulisho chako ili kukusaidia
wakati umepata matatizo.
Pia wakati wa kufanya mazoezi unatakiwa
utembee na glucose au sukari kwa ajili ya dharura,kwani unapofanya mazoezi bila
kula inapelekea kushuka kwa sukari.
Inatakiwa mgonjwa kufanya yote na kuzingatia utumiaji
wa dawa jambo litakalosaidia kuishi maisha marefu.
Mhana anasema kuwa jambo linalopeleka mgonjwa
anakatwa miguu ni kutokuwa na elimu kuhusu ugonjwa na kutofata
mashariti,hivyo serikali na wadau mbalimbali wenye ufahamu kuhusu kisukari watumie
muda mwingi kuwaelimisha.
Pia aliwataka wagonjwa kufata mashariti mpangilio wa
chakula, mazoezi, matumizi sahihi ya dawa na sindano za Insulini, na jamii
kuacha kuwa wavivu wa kufanya mazoezi ata kama haja athirika na kisukari pamoja
na ulaji wa vyakula vya kusindikwa viwandani.
Itaendelea, Imeandaliwa na Judith Ferdinand; 0757804962 Kwa msaada wa mtandao na mashirika ya habari.
No comments: