LIVE STREAM ADS

Header Ads

SOMA HAPA KUJUA UNACHOFIKIRI.

Kati ya vitu vigumu hapa duniani ni Kufikiri, na watu wengi huwa hawawezi kufikiri lakini wao hufikiri wanafikiri ila hawafikiri wanachanganya namna ubongo wao unavyofanya kazi na kufikiri. Watu hawa ndio huwa wanashindwa kutofautisha mawazo na kufikiri. Wanafikiri kama wana mawazo juu ya kitu fulani ndio wanafikiri.
Henry Ford aliwahi kusema "Thinking is the hardest thing there is that is why few people engage in it" yaani Kufikiri ni jambo gumu sana na ndio maana ni watu wachache sana ndio wanafikiri. Ukitaka kuamini watu hawafikirii pita kwenye vijiwe wanavyokaa sikiliza stori wanazopiga, maneno wanayoongea mimi huwa nayaita makelele ya wasiofikiri na utajua fika kama kweli wangekuwa wanafikiri wasingeongea wanachoongea.
Mtu anafikiri kwa picha na nimeandika mara nyingi sana hapa, ninaposema nyumba, gari, kuku,kijiko, friji, kitanda kinachokuja kwenye kiyoo cha akili yako ni picha ya hivi vitu na sio kitu kingine. Wakati hakuna picha halisi ya kitu mtu huwa haelewi vizuri kitu na huanza kufikiria mambo mengine hii ndio maana hata ukiwa unamwadithia mtu kitu fulani huwa unajitahidi kumwelewesha kwa picha na pia jiulize kwa nini watoto wadogo vitu vyao vya kujifunza ni vya picha picha tuu?
Mawazo huwa yanakaa kwenye akili na huwa hayalengi kutatua tatizo ambalo mtu anakuwa nalo kwa wakati huo lakini kufikiri kuzuri na ambako kunakuwa na tija huwa kunawekwa kwenye makaratasi au shajara sasa siku nyingine ukimuona mtu kashika tama anakuambia anafikiri mwambie pole wewe hufikiri bali una mawazo.
Tofauti nyingine kati ya mawazo na kufikiri ni kwamba mtu mwenye mawazo huwa anadumaza akali yake na kudhoofisha mwili wake ila mtu mwenye kufikiri huwa anapanua akili yake na fikra zake juu ya jambo fulani na namna mbalimbali anavyoweza kulitenda.
Mawazo mara nyingi mtu anakuwa nayo kutokana na matatizo fulani ambayo yanakuwa yamempata kwa kipindi fulani, lakini kufikiri huja kwa kutafuta namna ya kutatua jambo fulani ambalo linakutatiza moja kwa moja na sio kulipooza.
Tafiti zinaonesha kwamba 2% ya watu duniani ndio wanafikiri, 3% wanafikiri wanafikiri, 95% hawa hawataki kabisa kufikiri ni bora wafe kuliko wafikiri na hii ndio sababu katika dunia hii ni 5% ya watu wamefanikiwa na kufikia uhuru wa kifedha.
Kuna mtu alishawahi kusema kwamba tatizo la Africa halipo kwenye ardhi lipo kwenye kufikiri na huu ni ukweli mtupu, waafrika wengi hatufikiri hii ni kuanzia viongozi wanaotuongoza mpaka raia wa kawaida na hii ndio maana viongozi wanaamini wanaweza kuendelea kwa misaada na raia wanaamini kwenye kusaidiwa na serikali zao.
Sasa kama watu wengi hivyo hawafikiri wanafanya nini?
Wanashindwa kuelewa namna akili zao zinavyofanya kazi ni tofauti na kufikiri hivyo basi wanaruhusu kile ambacho macho yao yanakiona nje kutawala kilichopo ndani na hivyo wanasema wanafikiri. George Bernad Show aliwahi kusema "People are always blaming circumstance for what they are i don't believe in circumstances the people who make on this world are the people who went and look for circumstances that they want if they cant find them they make them"
Kwa nini nimeandika kuhusu kufikiri..
Ni kwa sababu mtu anakuwa kile anachofikiri kama unafikiri vibaya basi utapata matokeo mabaya na kama unafikiri vizuri utapata matokeo mazuri. Nabii Suleiman aliwahi kusema As the man thinketh in his heart so is he. Na hii ni kweli kabisa maana jinsi mtu unavyofikiri ndivyo utakavyotenda na ndivyo utakavyopata. Kuwa makini na namna unavyofikiri.
Unataka kujua nini unafikiri?
Sio kazi ngumu ni rahisi sana hebu angalia sehemu mbalimbali za maisha yako na matokeo unayoyapata, angalia kwenye mahusiano yako, biashara zako ni kiasi gani cha fedha unapata,ni kazi zako ni fedha kiasi gani unapata angalia na jifanyie tathimini hii itakueleza fika ni nini unachofikiri, na kama utakuwa na matokeo duni basi inamaanisha haufikirii vizuri unatakiwa kuanza kujifunza namna ya kufikiri vizuri ili uweze kupata matokeo makubwa zaidi.
Mada hii ya namna ya kufikiri, vyakula vya kutumia ili ufikiri vizuri,mambo ambayo yanamzuia mtu kutokufikiri vizuri,namna ya kubadili kufikiri kwako na vitu vya kufanya ili ufikiri vyema na ili niweze kufanikiwa inatafundishwa kwenye darasa letu la Whatsupp with Life secrets ( WWLF ) ambalo Litaanza awamu ya pili Tarehe 14/09/2015 ,ila wiki ya kwanza utasoma bure kwa audios na notes utapata hakikisha unajiunga ila hapa nimekumegea kitone cha darasa letu la WWLF .
LIKE PAGE YETU FACE BOOK LIFE SECRETS
Jiunge mapema wasiliana nasi 0689 452 670 email allnhump@gmail.com
KUMBUKA MAKALA ZETU UNAWEZA KUZISOMA BAADHI GAZETI LA MWANANCHI NA NYINGINE KWENYE BLOGS MBALIMBALI IKIWEMO BINAGI MEDIA BLOG, MJUMBE BLOG.
WALIO NA SHIDA YA KUANDIKA RESEARCH PROPOSALS, BUSINESS PLANS, FUND PROPOSALS AU ANDIKO LOLOTE WASILIANA NASI PIA.

No comments:

Powered by Blogger.