LIVE STREAM ADS

Header Ads

PRODUCER IBRAH DA BIZZY KUTOKA JIJINI MWANZA ASEMA KIONGOZI BORA HAPATIKANI KWA USHABIKI.

Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huu GB Pazzo akiwa pamoja na Producer na Director Ibrad da Bizzy (Kulia) kutoka Jijini Mwanza. Picha hii ina maana kuwa itikadi za Kivyama haziwezi kututenganisha Watanzania. 

Kumbuka ni katika Kampeni ya Mtandao huu (Binagi Media Group) iitwayo Piga Kura, Epuka Kula ambayo imelenga kuwahamasisha Watanzania kujitokeza kwa Wingi kushiriki katika uchaguzi wa Amani kwa Kupiga Kura na Kuwachagua Viongozi bora na si bora viongozi kwa ushawishi wa rushwa na ushabiki. Wanaobahatika kukutana na Mtandao huu hupata nafasi ya kutoa ujumbe wao kwa Watanzania wengine.

Ibrah anasema "Kiongozi Bora hapatikani kwa Ushabiki. Tanzania tunayoitaka iko mikononi mwetu hivyo Piga Kura, Epuka Kula kwa Maendeleo ya Taifa letu".
Binagi Media Group tunawaasa Watanzania Wasigawanyike kwa Misingi ya Itikadi za Kivyama. 
Tazama picha ya kwanza juu kisha ya pili chini utagundua kwamba Umoja ndio Msingi mkubwa wa Maendeleo ya Taifa letu na si itikadi za Kivyama.
Jua zaidi HAPA

No comments:

Powered by Blogger.