LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHINYANGA WATAKIWA KUTOWACHAGUA VIONGOZI WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA USHIRIKINA.

Na:Shaban Njia
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Saad Kusilawe amewaonya Wananchi wa Jimbo la Ushetu kuacha kuwachagua Wagombea Viti ambao wanajishirikisha na Imani za kishirikina katika kutafuta madaraka.

Kusilawe aliyasema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Ubunge  za Chama cha Mapinduzi (CCM)katika jimbo jipya la Ushetu zilizozinduliwa katika Kijiji cha Mseki Kata ya Bulungwa.

Katibu huyo alisema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya Wagombea wamekuwa wakijihusisha na imani za kishirikina ili kuhakikisha kuwa wanapata madaraka ya kuwaongoza Wananchi hali ambayo haiwezi kuvumiliwa na inapaswa kukemewa.

Katika uzinduzi huo Mgombea ubunge wa jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM Eliasi kwandikwa alihutubia Wanachi wa Jimbo hilo na kuahidi mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za Afya katika jimbo hilo pamoja na ujenzi barabara zinazounganisha jimbo la ushetu na Wilaya ya Urambo.

“Kwa mwaka huu wa uchaguzi tumechoka matusi kutoka kwa wagombea ubunge pia kwa kipindi cha nyuma tulikosa utashi kwa kiongozi tuliyempa madaraka kutuongoza katika jimbo la Kahama”. Alisema Kwandikwa.

No comments:

Powered by Blogger.