TOTO AFRICAN WATOSHANA NGUVU NA STAND UNITED KATIKA MCHEZO WAO WA KIRAFIKI.
Timu za Soka za Toto African (Bukta za Njano) Kutoka Jijini Mwanza pamoja na Stand United (Bukta ya Nyeupe) Kutoka Mkoani Shinyanga zimetoka sare ya 1-1 katika mchezo wao wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Ilemela Mkoani Mwanza.
Stand United (Wenye Bukta nyeupe) walikuwa wa Kwanza kuzichungulia nyavu za Toto African (Wenye Bukta za Njano) dakika ya 47 kupitia kwa nyota wao Hassan Seif Banda.
Bao hilo hata hivyo halikudumu muda mrefu kwani dakika ya 53 nyota wa Toto African Japhet Vedastus aliweza kusawazisha na hivyo kufanya matokeo hadi dakika ya 90 kuwa sare hiyo ya bao 1-1.
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii
No comments: