LIVE STREAM ADS

Header Ads

POLISI JAMII KUTOKA JUMUIYA YA MACHINGA KATIKA MASOKO NA MINADA JIJINI MWANZA WASHAURIWA KUTOTUMIKA.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akikagua gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Polisi Jamii kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara ndogondogo katika Masoko na Minada kwa Wilaya za Ilemela na Nyamagana.
Neema Emmanuel
Wahitimu wa mafunzo ya Polisi Jamii kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) katika Masoko na Minada Jijini Mwanza wametakiwa kuwa wazalendo na kutotumika kisiasa hususani katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu.

Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa Jeshi la Police Mkoa wa Mwanza, Kaimu Kamishina wa Polisi Charles Mkumbo, alipokuwa akifunga mafunzo ya polisi jamii kwa wanachama wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ndogondogo wa Minada na Masoko kwa Wilaya za Ilemela na Nyamagana katika Uwanja wa Magomeni Kirumba.

Aidha Kamanda Mkumbo alitoa rai kwa wahitimu hao kutambua kuwa ni wajibu wao kumlinda kila mmoja bila kujali chama, dini, kabila au itikadi za vyama vya siasa. 

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo Sajenti wa Polisi Mkoani Mwanza Clement Kabatila alisema kuwa wahitimu hao wamefundishwa ukamataji salama wa wahalifu, uzalendo, ukakamavu na upekuzi mambo yatakayowasaidia katika utendaji kazi wao. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Jastine Sagara alisema kuwa baada ya kero nyingi za uhalifu hususani katika Masoko na minada, umoja uliamua kuanzisha polisi jamii kwa lengo la kusaidia kukomesha vitendo hivyo.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa wa Kiyungi Magomeni Muhaji Iddy aliwatahadharisha wahalifu wote kuachana na vitendo vya uharifu ikizingatiwa kuwa wahitimu wa mafunzo hayo ya polisi jamii yamelenga kukabiliana nao.

No comments:

Powered by Blogger.