LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC KAHAMA APONGEZWA KWA KUTEKELEZA AHADI YA RAIS YA UJENZI WA BARABARA ZA RAMI.

Na:Shaban Njia
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Shinyanga kimempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Benson Mpesya kwa kusimamia vyema ahadi ya Rais Jakaya Kikwete juu ya ujenzi wa barabara za mji wa kahama kwa kiwango cha rami aliyoitoa kipindi cha mwaka 2010 alipokuwa na ziara ya kikazi katika Wilaya hiyo.

Hayo yalisemwa na katibu wa chama hicho Alhaji Saad katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika viwanja vya CCM tarafa ya Isagehe kwenye mji mdogo wa Kagongwa Wilayani Kahama.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya hiyo Benson mpesya alisema aliamua kulivalia njuga suala la ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ambayo ilikuwa ni ahadi ya Rais Kikwete aliyoitoa kwa wananchi wa Kahama ili isije ikawa aibu kwake kwa kuwa yeye ndiye msimamizi wa Wilaya hiyo kwa niaba ya Rais.

“Hadi nakamilisha ujenzi wa Barabara hizi kwa kiwango cha rami niliweka mahusiano mazuri baina ya Serikali na kampuni ya Acacia kupitia mgodi wake wa Dhahabu wa Buzwagi walitusaidia,licha ya kukamilisha barabara hizo pia Buzwagi wamepanga kutuwekea taa za kuongoza magari barabarani pamoja na taa mji mzima,”alisema Mpesya.

No comments:

Powered by Blogger.