LIVE STREAM ADS

Header Ads

ESTHER MATIKO AWAAHIDI NEEMA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO WA DHAHABU WILAYANI TARIME.

"Tunamshukuru Mola juzi tuliweza kufanya kampeni za kuomba kura kata ya Kenyamanyori mtaa wa Kibaga ambapo Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini (Chadema) Esther Nicolaus Matiko alipata pia nafasi ya kuwatembelea wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu katika Kata hiyo (Kebaga Mining)
Katika kunadi sera Matiko aliwaahidi wachimbaji hao kuwa ataendelea kuwatetea na kuwapigani kama anavyofanya kwa wachimbaji wadogo wadogo na wafanyakazi wa Mgodi wa Nyamongo (Acacia Gold Mining).
Aliwaahidi kuwawezesha kwa kuwapa mikopo yenye riba nafuu ili wajiendeleze katika shughuli zao za uchimba wa madini.
Pia Matiko aliwaahidi kuwapatia Mashine ndogo ndogo Mfano Procesing Table (PT), Mashine ya kukoboa Mawe (Grendar) pamoja na Mashine ya kusaga Kokoto zitakazowaweza kufanya kazi katika Mazingira salama tofauti na Mazingira ya sasa wanayofanyia kazi mfano kusafisha dhahabu kwa kutumia mikono kwenye maji yaliyochanganywa na Mercury pia kuponda kokoto kwa kutumia nyundo ndogo.
Matiko aliwaahidi wananchi wa kata ya Kenyamanyori kuwa atatumia eneo liliotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya secondari kujenga shule ya Bweni ya Wasichana itakayokuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita hii ni kutokana na Wilaya nzima ya Tarime kuwa na shule moja tu ya bweni ya A Level (Tarime secondari) inayopokea wanafunzi wa kiume tu.
Hali hiyo imesababisha wilaya ya Tarime kuwa nyuma kwa kusomesha watoto wa kike, kama ambavyo watoto wengi wa kike wamekuwa wakimwita yeye ni mfano wao wa kuigwa (Role Mode).
TARIME YETU, MSHIKAMANO KWA WOTE. RASIRIMALI ZETU, KWA MAENDELEO YETU.
ESTHER MATIKO, MBUNGE TARIME MJINI 2015".
Imeandikwa na Peter Magwi Michael-Team Matiko
BINAGI MEDIA GROU, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII

No comments:

Powered by Blogger.