LIVE STREAM ADS

Header Ads

ESTHER MATIKO NI MOTO WA KUOTEA MBALI JIMBO LA TARIME MJINI.

Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini Esther Nicolaus Matiko akiwahutubia mamia ya wakazi wa jimbo hilo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mpira Serengeti Kata ya Sabasaba
Na:Peter Magwi Michael
Team Matiko kwa kipekee kabisa tunamshukuru Mola kwa kuwa nasi tangu asubuhi tulipoanza siku ya leo (jana) kwa kutafuta kura kwa kuanzia makundi kadhaa.
Pia kwa niaba ya Team Matiko napenda kuwashukuru wale wote waliowezesha mikutano yetu miwili ya Kampeni kufanikiwa na kumalizika salama.
Licha ya siku ya leo (jana) kuwa na mvua nyingi ya mawe ilitulazimu kufanya Kampeni huku tukinyeshewa ili kuhakikisha kuwa wanawanchi wa Tarime wanaielewa Ilani ya Esther Nicolaus Matiko (Chadema) ambae ni mgombea ubunge Jimbo la Tarime Mjini.
Tulianzia na Kata ya Kitare Mtaa wa Romoli kisha tukarejea Kata ya Sabasaba na kufanya mkutano mkubwa ulioambatana na uzinduzi wa Kampeni za Mgombea udiwani katika Kata hiyo Hamisi Nyanswi uliofanyika viwanja vya Serengeti maarufu kwa jina la Shamba la bibi.
Wananchi wa Tarime tunawashukuru sana kwa kutusindikiza kwa Miguu baada ya mkutano wetu wa leo (jana) kutoka viwanja vya sabasaba mpaka ofisi za chama wilaya (Chadema) kwa shangwe na furaha nyingi.
Wananchi wa Tarime wako tayari kwa Mabadiliko, tusisite kuwasisitizia ndugu zetu watembee ndani ya Mabadiliko haya kwa Maendeleo ya Tarime kwa Kuwachagua Madiwani wote wanane wa kata zote za Tarime Mjini (Chadema), Esther Nicolaus Matiko kuwa mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Edward Ngoyai Lowasa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tulianza na Mola, Tutamaliza na Mola.
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini Esther Nicolaus Matiko akiwahutubia mamia ya wakazi wa jimbo hilo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mpira Serengeti Kata ya Sabasaba
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Lucas Ngoto akiwaombea kura wagombea wa Ukawa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mpira Serengeti Kata ya Sabasaba
Mgombea Udiwani Kata ya Sabasaba Jimbo la Tarime Mjini Hamis Nyanswi kupitia Chadema akiomba kura katika Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Mpira Serengeti Kata ya Sabasaba
Wakazi wa Tarime Mjini
Mamia ya wakazi wa Jimbo la Tarime Mjini waliohudhuria Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu katika Kata ya Sabasaba jimboni huo
Mamia ya wakazi wa Jimbo la Tarime Mjini waliohudhuria Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu katika Kata ya Sabasaba jimboni huo
Mgombea ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia Chadema Esther Matiko (Nwenye Kofia) akiwa pamoja na viongozi wengine wa chama, akisindikizwa kuelekea zilipo ofisi za chama Wilaya ya Tarime baada ya kutamatika kwa mkutano wa jana katika Uwanja wa Serengeti

Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Tarime Lucas Ngoto akiteta jambo na Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia Chadema Esther Matiko (Mwenye Kofia). Anaefuata ni Hamis Nyanswi ambae ni Mgombea Udiwani Kata ya Sabasaba kupitia Chadema

No comments:

Powered by Blogger.