LIVE STREAM ADS

Header Ads

JE UNAJUA KUWA MASIKINI NI DHAMBI? SOMA HII HAPA.

Watu waliofanikiwa kuna mambo fulani ambayo huwa wanayafanya kila siku na kwa sababu ni tabia yao basi hujikuta wanafanikiwa kila iwapo leo. Lakini na masikini pia nao huwa wana mambo fulani ambayo nao huwa wanayafanya kila siku na kwa sababu ni tabia yao nao huendelea kuwa masikini kila iwapo leo.
Mafanikio siyo kitu walichoumbiwa watu wa jamii fulani tuu au kabila fulani bali ni kitu ambacho Mungu alimuumbia kila mtu. Na Mungu anapenda kumuona binadamu akiendeleza uumbaji wake, maana Mungu ndiyo asili ya uumbaj, kwa maana nyingine mafanikio ni utukufu kwa Mungu na Mungu anapenda kuona watu wakifanikiwa, wakiishi maisha ya furaha na amani na sio vinginevyo.
George Bernad Show mwandishi wa mashairi ambaye aliwahi kushinda tuzo ya Nobel miaka ya 1923 aliwahi kusema sentensi mbili ambazo ziliwafanya watu wabaki midomo wazi na kumshangaa na wengine kumkatalia maneno yake na kusema anadharau, leo naomba nimnukuu tena...
Sentensi ya kwanza It is a sin to be poor (Ni dhambi kuwa masikini) Sentensi ya pili It is a duty to every person to be rich(Ni sharti kwa kila mtu kuwa tajiri).
Ili kuweza kumuelewa vizuri Bernard Show kwanza ni lazima uwe na (open mind), maarifa ya kutosha na msomaji mzuri wa vitabu mbalimbali vya maendeleo binafsi pamoja na vitabu vya dini.
Mtu anaezijua sheria vizuri akazifanyia kazi pasipo kuzivunja ni lazima atapata mafanikio ,lakini asiezijua na anaezivunja atakuwa masikini tuu.Sheria nazoongea hapa ni sheria ya kupanda na kuvuna, sheria ya kuvutia, sheria ya mvutano, sheria ya kuheshimu n.k Hivyo alichokisema George Bernad show ni kitu cha ukweli kabisa na chenye mantiki kwa kufuata sheria.
Isitoshe Mwandishi Mathayo wa Agano jipya nae alisema maneno hayo hayo miaka mingi iliyopita kabla hata ya George Bernad show alisema kwamba "yule alienacho kidogo atanyang'anywa na atapewa yule mwenye vingi" kwa maana nyingine anachosema hapa ni kwamba masikini ataendelea kuwa masikini na tajiri kuwa tajiri, sasa kama uelewa wako ni mdogo utaona huu ni uonevu lakini hapana ngoja nikuambie kwa nini..
Masikini ambaye anaongelewa hapa ni masikini wa kufikiri, kama hufikiri vizuri ina maana utafanya vibaya na utapata matokeo mabaya na hata kitu ulichokuwa nacho saizi kuna uwezekano wa wewe kukipoteza, hivyo basi ataongezewa yule ambaye tayari anakitu hivyo atazidi kutajirika,umasikini wa kufikiri unamfanya mtu kusikia, kunusa,kuona,kutembea sawia na umasikini alionao kwenye akili yake.
Kitakachofanya alienacho azidi kuongezewa ni fikra zake zinafikiri juu ya mafanikio na kulingana na sheria ya kuvutia atapata kulingana na anachofikiri hivyo atazidi kuongezewa zaidi na atazidi kuwa tajiri, Masikini nae atalipwa sasa sawa na ujira wake atawaza mawazo ya kushindwa, atatenda vibaya maadamu kawaza vibaya na atavuna vibaya hivyo hata kile alichokuwa nacho atakipoteza.
Umasikini humfanya mtu asiweze kujiamini na kujitegemea peke yake hivyo humfanya binadamu kumtegemea binadamu mwenzake, kumbuka tena imeandikwaje? Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu mwenzie tayari umefanya dhambi. Tegemeo la kweli linatoka kwa Mungu tuu binadamu hawaaminiki na wanabadilika badilika.
Lakini pia umasikini humfanya mtu kuwa mwoga na kutokujiamini na si unakumbuka njia pekee ambayo Shetani anamtawala mtu ni kupitia woga anaokuwa nao juu ya kitu fulani, watu wanaoishi kwa hofu ya ugonjwa au jambo fulani ndio wanaoishia kupatwa na ugonjwa huo au jambo hilo kutokea kwenye maisha yao.
Ukweli ni kwamba Shetani hutawala watu ambao hawafikiri vizuri na ambao wana woga, ukiwa unafikiri vizuri na huna woga kamwe huwezi kutawaliwa na Shetani kwa sababu Shetani ni nguvu pinzani na Mungu. Unakumbuka Ayubu alisemaje wakati Shetani kaanza kumjiribu?alisema vitu ambavyo nilikuwa naviogopa vimeanza kunitokea. Shetani ni nguvu hasi kama unataka kumshinda ni kuwa na Nguvu Chanya ambayo ni ya Mungu tuu.
SHEA UJUMBE HUU KADRI UWEZAVYO.
WHATSPIKA WITH US 0689 452 670. DARASA LITAANZA AWAMU YA PILI TAREHE 14/09/2015 JIANDIKISHE MAPEMA UTASOMA BUREE WIKI YA KWANZA.
email allnhump@gmail.com

No comments:

Powered by Blogger.