LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA NNE: HATUA SITA MUHIMU MTU ANAZOTAKIWA KUPITIA ILI KUFANIKIWA.

Soma HAPA Sehemu ya Tatu
HATUA YA NNE NI KUANZA
Baada ya kupanga hatua ambayo inafuata ni kuanza kutenda yale uliokuwa umeyapanga. Hiki ni kipindi ambacho unatoa mambo ulioandika kwenye makaratasi na kuyafanyia kazi, Kuanza kufanya inamaanisha kwamba kile ulichokipanga unataka kukiona kinatimia katika maisha yako, Hii ni hatua muhimu sana kwani hata kama umepanga vizuri kiasi gani ila kama usipoanza inamaanisha hicho ulichokipanga hakitakaa kitokee milele.
Siku ambayo utaanza kufanya jambo lako basi ni siku ambayo utakuwa na shauku na nguvu ya ajabu, ulipanga kwamba utaenda kusoma elimu ya miamba sasa upo darasani kwa siku ya kwanza mwalimu anafundisha nawe unasikiliza na kuandika kile unachofundishwa hii ni siku nzuri na yenye nguvu ya ajabu, ulikuwa umepanga kufungua duka la vipodozi sasa umeanza mteja wa kwanza anakuja unamuhudumia na wa pili na wa tatu ,ulikuwa unataka kupunguza uzito unaanza mazoezi, kuzingatia mlo kamili hapa akili na mwili wako huwa vinajisikia vizuri sana.
Siku ambayo unaanza kufanya kile ulichokuwa umekipanga ndio siku ambayo unakuwa umejiingiza katika uelekeo mpya kwenye maisha yako haimaanishi kwamba kwa sababu umeanza basi ni lazima utapata kile unachokitaka, mambo yanaweza yakaenda kinyume na ulivyopanga lakini haupaswi kukata tamaa unatakiwa kuendelea kufanya zaidi na zaidi kwa sababu unaamini kile ulichokipanga kwamba kinawezekana ndipo ule msemo wa kadiri navyofanya kazi kwa bidii ndivyo navyokuwa na bahati utafanya kazi kwako.
Usithubutu kuanza kabla ya kupanga maana utashindwa kufikia lengo lako, Sababu kubwa ya watu kushindwa katika maisha ni kwamba wananza kufanya vitu mbalimbali pasipo kupanga, na pia sababu nyingine ya watu kushindwa ni kwamba wanapanga vitu pasipo kuvifanyia kazi mtu anaeanza kufanya kitu bila mpango hata tofauti na mtu anaepiga risasi hewani bila shabaha ni dhahiri kamba atakuwa anapoteza muda wake na hakutakuwa na madhara yoyote.
Kuna msemo wa Kiswahili ambao unasema mwanzo ni mgumu hii ni kweli kabisa na isikukatishe tamaa unatakiwa kuendelea kujisukuma kufanya zaidi na zaidi ili kuweza kufikia lengo lako, sasa sijaandika kukukaririsha na kukutishia kwamba mwanzo ni lazima uwe mgumu ila kwa kiasi kikubwa ni lazima uwe na ugumu lakini kiwango cha ugumu huwa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine ni lazima uwe na ujasiri wa kuvumilia na kujisukuma katika kile ambacho unakiamini wengi huwa wanaacha kwa sababu wanakosa uvumilivu.
Kuanza kuna faida nyingi sana kwa mtu ambaye tayari ameshapangilia mambo yake, kuanza inamaanisha kwamba kile ulichokipanga kiaanza kupata kuonekana nje na kinaanza kupata muonekano maana kipindi unapanga kilikuwa kipo kwenye makaratasi na hakikuwa kinaonekana kwa watu.
Kitendo tuu cha wewe kuanza huwa kinakukutanisha na watu wengine ambao wanafanya kitu kama hicho na pia unaweza ukajifunza kutoka kwao au ukatengeneza urafiki na wao hivyo ukaongeza idadi ya marafiki..Ni wote tunajua kwamba ili kufanikiwa zaidi unahitaji watu na hao watu hakuna namna utawapata kwa kukaa nyumbani ni mpaka uanze kufanya kitu fulani ulichopanga
Kuanza kunamfanya mtu apate kujua kwamba ule mpango aliokuwa kaupanga kama anaweza kuufanyia kazi au laa na kama ataona kwamba hauleti matokeo mazuri basi anakuwa katika hatua nzuri ya kuubadilisha mpango huo na kutengeneza mpango mwingine, huwa tunabadili mpango sio wazo na ni nadra sana watu wenye tabia ya kubadili badili mawazo wakafanikiwa.
Lakini pia kuanza inamaanisha haupo tayari kwenda kufanya mambo mengine zaidi ya yale uliyoyapanga hii inamaanisha muda, nguvu na akili zako zote utazielekeza kwenye mambo ambayo umeyapanga. Ni mara chache sana watu wenye tabia ya kuanza jambo moja na kuacha wakarukia jingine na kuacha wanafanikiwa,njia yenye uhakika ya kufanikiwa ni kuanza jambo moja na kulisimamia mpaka uone limekamilika ndipo unaanzisha jingine.
Nenda kaanze kile ulichokuwa umekipanga usikubali tabia ya kuhairisha kukusababisha kutotenda kile ulichokipanga, anza sasa maana muda uliokubalika ni leo watu wenye tabia ya kuhairisha mambo huwa wanakosa fursa mbalimbali katika maisha. Anza hapo ulipo kwa kile ulichonacho hata kama ni kidogo, Jack Ma anasema "start small provide wonderful service with least cost having big vision in your dream" yaani anza kidogo toa huduma bora kwa gharama ambayo ni ya chini lakini uwe una maono makubwa katika kile ulichoanzisha.
Itaendelea
SIKU NJEMA...SHEA NA WENZIO WENGI KADIRI UWEZAVYO LIFE SECRETS COMPANY!

No comments:

Powered by Blogger.