LIVE STREAM ADS

Header Ads

UKAWA WARINDIMA JIMBO LA TARIME MJINI. WANANCHI WANUSURU TIMBWIRI LA CHOPA.

Mgombea Ubunge kupitia Chadema katika Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko juzi akiwahutubia wakazi wa jimbo hilo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nyamisangura.
Na:Peter Magwi-Team Matiko
Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar Salum Mwalimu pamoja na viongozi, makada na wagombea wa chama hicho akiwemo James Lembeli.

Katika mkutano huo, wananchi walichanga fedha kiasi cha shilingi Laki Saba na Elfu Arobaini na Mia Tano (740,500) kwa ajili ya malipo ya chopa iliyokuwa inatumiwa na viongozi wa chama baada ya kutokea mvutano katika hotel ambayo chopa hiyo ilila ambapo fedha iliyokuwa ikihitajika ni shilingi Laki Tano (500,000) huku habari zikieleza kuwa meneja wa hotel hiyo aliwekwa kitimoto hadi pesa hizo zilipwe.
Wakazi wa Jimbo la Tarime Mjini wakizungusha mikono kama ishara ya MABADILIKO
Wakazi wa Tarime Mjini wakiwa katika Mkutano wa UKAWA katika Uwanja wa Nyamisangura
Wakazi wa Tarime Mjini wakiwa katika Mkutano wa UKAWA katika Uwanja wa Nyamisangura
Wakazi wa Tarime Mjini wakiwa katika Mkutano wa UKAWA katika Uwanja wa Nyamisangura
Naibu Katibu Mkuu Chadema kutoka Zanzibar Salum Mwalimu akiwahutubia wakazi wa Jimbo la Tarime Mjini
Naibu Katibu Mkuu Chadema kutoka Zanzibar Salum Mwalimu akiwahutubia wakazi wa Jimbo la Tarime Mjini
Mgombea ubunge jimbo la Kahama Mjini Mkoani Shinyanga James Lembeli akiwahutubia wakati wa Jimbo la Tarime Mjini
Mgombea ubunge jimbo la Kahama Mjini Mkoani Shinyanga James Lembeli (Kulia) akimwombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko kwa ishara ya kumshikisha fimbo ya kitemi
Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko akichangisha pesa kwa ajili ya kulipia hotel ilikolala chopa
Katibu Mkuu Chadema Zanzibar Salum Mwalimu akichangisha pesa kwa ajili ya kulipia hotel ilikolala chopa
Pesa zilizochangwa na wananchi zikihesabiwa ambapo zaidi ya Shilingi Laki Saba zilipatikana.
Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko akiingia katika Chopa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Tarime Mjini Lucas Ngoto
Chopa ikiondoka eneo la Mkutano

No comments:

Powered by Blogger.