LIVE STREAM ADS

Header Ads

TATIZO LA WAJAWAZITO KULALA WATATU KITANDA KIMOJA KUTAFUTIWA UFUMBUZI MJINI KAHAMA.

Na:Shaban Njia
Changamoto ya akinamama wajawazito kulala watatu katika kitanda kimoja inatarajia kupungua katika hospitali ya Wilaya ya Kahama kutokana na shirika lisilo la kiserikali la One Person Project kutoka nchini Canada kutoa kiasi cha shilingi Milioni moja na nusu kwa ajili ya uboreshaji ya miundo mbinu katika wodi ya wazazi hospitalini hapo

Akikabidhi fedha hizo jana Mwakilishi kutoka shirika hilo Emmanuel Mlau alisema kuwa shirika lake limeamua kutoa msaada huo kwa lengo la kuboresha Miundombinu katika wodi kama ununuzi wa vitanda pamoja na vifaa tiba vya kujifungulia.

Alisema kuwa wametoa fedha hizo baada yawazazi kukosa vifaa vya kujifungulia na kuongeza kuwa shirika hilo limetanga dolla 1000 kwa ajili ya ukalishwaji ya miundombinu iliyopo katika wodi hiyo hali ambayo itapunguza vifo visivyo vya lazima kwa akinamama wajawzito hasa wakati wa kujifungua.

“Hali ya hospitali ya wilaya Kahama ni nzuri,shirika limeona nivizuri likaamua kuwasaidia msaada huo ili kuboresha wodi ya wazazi hali ambayo itasaidia katika mambo mbalimbali kama ununuzi wa vitanda pamoja na vifaa kwani tunatambua kuwa vifo vya akinamama vitapungua kwa kiasi Fulani” alisema Mlau.

Kwaupande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Fredrick Malunde alisema kuwa Msaada huo ambao umetolewa na shirika la One Person Project utasaidia kupunguza changamoto zilizopo katika wodi ya akinamama wajawazito pamoja na ununuzi wa vifaa tiba.

Pia ametoa wito kwa mashirika mengine kujitoa kama shirika la One Person Project kwani hospitali hiyo imekuwa na changamoto hasa wodi ya wazazi ambayo imekuwa na ongezeko kubwa la wazazi akinamama wajawazi wanaotoka umbali mrefu ikiwa ni sambamba na wilaya jirani.

“Hospitali ya Wilaya ya Kahama imekuwa na ongezeko la wagonjwa hasa wajawazito kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo wilaya jirani za Urambo,Geita,Nzega pamoja na Nyang’wale hali inayofanya wajawazito hao kulala kitanda kimoja watu wawili hadi watatu hivyo fedha hii inaweza kupunguza adha hiyo” alisema Kaimu Mganga Mkuu.

Aidha Malunde aliyataka mashirika mengine kuguswa na hali ya hospitali hiyo nakuongeza kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kuporesha katika huduma za afya hivyo jitihada nyingine zinatakiwa kuonyeshwa na mashirika mengine ikiwa ni sambamba na watu wenye mapenzi mema kusaidia sekta ya afya.

No comments:

Powered by Blogger.