WAKAZI WA MWANZA WATAKIWA KUZINGATIA UTUNZANI WA MAZINGIRA.
Na:Vesterjtz,Mwanza
Wakazi
wa Mkoa wa Mwanza wametakiwa kutunza mazingira ili kujikinga na maradhi
ya milipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu hususani katika msimu huu
wakipindi cha mvua na msimu wa maembe.
Akizungumza jana, Mratibu wa mradi wa Mwanza Tampere na
Mazingira Amin Abdarah alisema jamii imekuwa ikishindwa kutunza mazingira
ipasavyo na kusababisha magohnjwa ya milipuko hususani gonjwa la
kuhara.
“Jukumu la kutunza mazingira ni la kila
mtu na sio serikali pekee,magonjwa ya mambukizi kama kipindupindu ni
jukumu la kila mwananchi kuhakikisha Tanzania inaondokana na magonjwa
yanayoepukika,”alisema Amini.
Hivyo jamii inapaswa
kuzingatiumuhimu wa usafi na kuwepo kwa maji safi ya kunywa
kusafisha vyombo kwa maji safi na salama kutumia sabuni kwa kunawa
mikono,uhifadhi wa chakula na vyoo bora na kusafisha maeneo
yanayowazunguka.
Aidha maradhi ya kipindupindu
yamewahi kuripotiwa mara nyingi kuzuka sehemu mbalimbali duniani
kulingana na shirika la afya ulimwenguni WHO watafiti wanakadilia kuwa
kati ya watu milion1.4 hadi milioni 4.3 huripotiwa kuugua kipindupindu
huku elfu 142 hupoteza maisha kila mwaka kwa ugonjwa huo ambao
huwaathiri watoto na watu wazima.
Mwisho.
No comments: