LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MWENEZI WA CCM WILAYANI KAHAMA AMTUHUMU KHAMIS MGEJA.

Khamis Mgeja
Na:Shaban Njia
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Masoud Melimeli amesema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani humo Khamis Mgeja ambae ametimkia Muungano wa Upinzani UKAWA ni mmoja kati watu waliokifirisi Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU).

Melimeli aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia wakazi wa Mji wa Kahama katika Mkutano wa Kumnadi Mgombea Udiwani kata ya Kahama Mjini (CCM)Hamidu Kapama.

“Nawaambieni mwaka 2000 aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg.Benjamini Mkapa alitaka kuivunja Halmashauri ya Wilaya Kahama kutokana na wizi uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo ambapo Mwenyekiti wake alikuwa ni Khamis Mgeja”. Alisema Melimeli.

No comments:

Powered by Blogger.