LIVE STREAM ADS

Header Ads

UKAWA KUFUNGA KAMPENI ZAKE KATIKA UWANJA WA MBUGANI JIJINI MWANZA KWA HISTORIA?

Jumamosi Octoba 24,2015 ni siku ambayo itakuwa na mikiki mikiki ya hapa na pale katika Viwanja mbalimbali nchini ambapo Vyama kadhaa vya Siasa vitakuwa vikifunga Kampeni zake ikiwa ni katika kuelekea kesho jumapili Octoba 25 ambayo ni siku ya Uchaguzi Mkuu nchini kwa ajili ya Watanzania kuwachagua wawakilishi wao kuanzia Madiwani, Wabunge na Rais.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza, Mh.Frederick Sumaye anatarajiwa kufunga Kampeni za Chama cha Maendeleo Chadema na hivyo kuwaombea kura wagombea wa Majimbo mawili ya Ilemela (Highness Kiwia) na Nyamagana (Ezekiel Wenje) katika dakika za lala salama kubwa zaidi ikiwa ni kujua nani zaidi kati ya CCM na Ukawa Jijini Mwanza ikizingatiwa kuwa pande zote mbili zinafunga kampeni zake hii leo.

Mkutano huo unatariwa kuwa na amsha amsha za kutosha pia kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya pamoja na Bongo Movie maarufu kwa jina la Team Mabadiliko.

Kama hiyo haitoshi, Kitaifa Chama cha Mapinduzi CCM kinatarajia kufunga kampeni zake hii leo katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo mbali ya Mgombea Urais Dkt.John Pombe Magufuli na Mgombea mwenza wa Urais Mama Samia Hassan Suluhu kuhudhuria Mkutano huo, pia viongozi mbalimbali wa chama akiwemo mwenyekiti wake Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wanatarajiwa kurindima uwanjani hapo.
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII TUNAHIMIZA AMANI KATIKA UCHAGUZI MKUU 2015.

No comments:

Powered by Blogger.