LIVE STREAM ADS

Header Ads

KISHIMBA AMKEJELI LEMBELI JUU YA MATUMIZI YA MFUKO WA JIMBO.

Na:Shaban Njia
MGOMBEA Kiti cha Ubunge katika jimbo Jipya la Kahama Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Jumanne Kishimba amemtaka aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembeli kuorodhesha Matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Wananchi kwa kipindi cha Miaka kumi ya uongozi wake na akifanya hivyo atamlipa gharama ya milioni 10.

Kishimba aliyasema hayo kwa nyakati tofauti alipokuwa akiwahutubia Wanachi wa Kata ya Nyasubi Mjini Kahama na Kijiji cha Bujika katika Kata ya Nyandekwa na kuongeza kuwa Kama Lembeli ataeweza kuwaleza Wananchi matumizi ya fedha hizo atamlipa kiasi hicho cha fedha.

Akiwa katika kata ya Nyasubi Mjini Kahama Kishimba alisema kuwa anasikitishwa na baadhi ya Wabunge wanapokuwa madarakani kutowatendelea haki Wananchi ikiwa ni sambamba na kutowashirikisha katika matumizi ya fedha za Mfuko wa jimbo zinazitolewa na Bunge kila mwaka.

“Mimi nikiingia madarakani hata mkiteuwa Wawakilishi wenu kuzisimamia fedha hizo mimi nipo tayari na siwezi hata siku moja kula fedha za mfuko wa Jimbo ambazo kimsingi ni mali ya Wanaanchi unaowaongoza”. Alisema Kishimba.

Hata hivyo Kishimba alisema kuwa Wananchi wa Jimbo lililokuwa la Kahama katika kipindi kilichopita hawakuweza kuona miradi yeyote ya maendeleo ikiibuliwa kupitia Mbunge aliyekuwepo madarakani licha ya kupewa kiasi cha shilingi milioni 750 kama mfuko wa jimbo lake ili kuweza kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata alizokuwa akiongoza.

Aidha Mgombea Ubunge huyo akiwa katika kata Kijiji cjha Bujika katika kata ya Nyandekwa aliwaahidi wanachi kuwajengea Zahanati ikiwa ni sambamba na kuwaletea Madaktari Wastaafu pamoja na Wauguzi huku wakisubiri zahanati inayojengwa kwa nguvu za Serikali kukamilika.

Alisema kuwa katika kata ya Nyandekwa kuna ujenzi wa Zahanati unaendelea lakini Wananchi hawawezi kusubiri mapaka Ikamilike huku watu wakiuugua kila siku na kuongeza kuwa kutoaka na hali hiyo hana budi kuanzisha huduma hiyo ya matibabu kwa kukodi majengo pamoja na Madaktari na Wauguzi kwa ajili ya kundeleza huduma hiyo.

Pia Kishimba aliwataka Wananchi pamoja na kuwa katika matabaka ya vyama tofauti tofauti kuhakikisha kuwa tarehe 25 ikifika wanachagua kiongozi mzuri anayeongoza na sio kuchagua chama hali ambayo itachangi kwa kiasi kikubwa katika kuonyesha ukomavu wa kidemokrasia.

No comments:

Powered by Blogger.