LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAHABARI WAASWA KUTOFUNGAMANA NA VYAMA VYA SIASA

Na:Shaban Njia
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Kahama Mabala Mlolwa amewataka Waandishi wa Habari Wilayani hapa katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu kuhakikisha kuwa wanaandika habari kwa kufuata weledi wa taaluma yao na si kupotosha jamii.

Mlowa aliyasema hayo katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba katika Kampeni zinazoendelea katika kata ya Nyasubi Wilayani hapa.

Alisema kuwa Waandishi wa Habari ni kama kioo cha jamii na kitu chotechote kinachotangazwa kupitia wao jamii huamini kwa kiasi kikubwa hali ambayo kama watapotosha kunaweza kusababisha kuvunjika kwa amani katika eneo husika.

“Nina waomba Waandishi wa Habari kuhakikisha kuwa mnaandika habari za kweli na sii kupotosha jamii na hata katika machafuko ya nchi za Burundi na Rwanda baadhi ya Waandishi wa Habari waliweza kukamatwa na kufikishwa mahakani kwa ajili ya kuandika habari za uchochezi”. Alisema Mlolwa.

Aidha aliendelea kusema kuwa licha ya baadhi ya Waandishi wa Habari kupata mafunzo ya kuandika habari zinazohusu uchaguzi Mkuu lakini kuna baadhi yao wamekuwa wakienda kinyume na mafunzo kwa kuandika habari zisizo za ukweli na kuipotosha jamii husika.

Hata hivyo katika Mkutano huo Mwenyekiti huyo alitumia muda huo kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba huku akiwataka Wananchi kumchagua ili aweze kuleta maendeleo katika Jimbo Jipya la Kahama Mjini.

Alisema kuwa Kishimba ni Mzaliwa wa Kahama na Mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa na kuongeza kuwa kama Wananchi wa Jimbo la Kahama Mjini watamchagua ataweza kuwaletea maendeleo hasa katika sekta ya Biashara kwa kutumia uozefu wake alio nao tangu miaka ya nyuma.

Nae Jumanne Kishimba akiongea na Wananchi alisema kuwa amekuwa akibezwa na baadhi ya Wagombea kuwa hajui kuongea kwani hata akifika Bungeni atakuwa akikaa kimya na hivyo kushindwa kujenga hoja kwa Wananchi wake katika mijadala mbalimbali.

“Mimi wanasema sijui kuongea mbona Mgombea Uraisi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dr, John Magufuli alipokuja nilimuomba barabara za lami katika Mji wa Kahama zenye urefu wa kilometa tano na kisha aliniongeza tano nyingine zikawa kumi, na pia nilimwomba kupandishwa hadhi kwa Hospitali ya Wilaya kuwa ya Rufaa na alikubali,je mimi sijui kuongea?". Alihoji Kishimba na kuongeza;

“Mbona Dr.Magufuli alisema kuwa toka alipokuwa na Mbunge aliyemaliza Muda wake kwa kipindi cha Miaka kumi lakini hajawahi kumuomba barabara hata kilometa moja, je, Mimi na yeye nani hajui kuongea? Alisisitiza Kishimba.

No comments:

Powered by Blogger.