KISHIMBA ASHUSHA AHADI KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA NA MATUNDA MJINI KAHAMA.
Na:Shaban Njia
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kahama mjini Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Jumanne Kishimba amewaahidi neema wakulima wadogowadogo wa matunda na mbogamboga kwa kuwatafutia fursa ya kuuza bidhaa mazao yao katika mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya Acacia.
Kishimba alitoa ahadi hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi wa mji wa Kahama katika mdahalo wa wagombea Ubunge wa jimbo hilo.
Kishimba alitoa ahadi hiyo alipokuwa akijibu swali la mmoja wa washiriki wa mdahalo huo Leonald Gilitu aliyetaka kujua namna atawasaidiaje wakulima wadogowado wa matunda na mboga mboga kupata fursa ya kuuza bidhaa zao katika mgodi wa Buzwagi ambao umekuwa ukituhumiwa kufanya biashara hizo na wafanyabiashara kutoka nje ya mkoa wa Shinyanga.
“Ninafahamu kuwa wapo wakulima wanaolima mazao ya mboga mboga na matunda lakini hawapati fursa ya kuuza mazao hayo mgodini hali ambayo inachangia yanaharibika kutokana na kukaa muda mrefu sokoni na hivyo kuingia hasara”. Alisema Kishimba.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge kwa tiketi ya ACT wazalendo Bobson Wambura ambaye pia alihudhuria mdahalo huo aliwataka wananchi kukubali matokeo ya mgombea yoyote atakaechaguliwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho kutwa octoba 25.
No comments: