LEMBELI AKANUSHA KULIKIMBIA JIMBO BAADA YA KUUKOSA UBUNGE.
Na:Shaban Njia
Aliekuwa mgombea Ubunge katika Jimbo jipya la Kahama Mjini Mkoani Shinyanga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA James Lembeli amesema kuwa ataonekana katika jimbo hilo kwa muda wa wiki mbili na baada kusafiri kwenda nje ya nchi kupumzika kutokana na mchuano mkali alioupata kwa mpinzani wake aliyeshinda kiti hicho kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Jumanne Kishimba.
Lembeli ambae msimu uliopita alikuwa mbunge wa jimbo hilo akiwa CCM, aliyasema hayo juzi kupitia radio yake iliyopo mjini Kahama na kuongeza kuwa katika uchaguzi huo hakutendewa haki ambapo aliwatupia lawama wasimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo kwa kutotenda haki.
“Bado niko jimboni kwangu na ashangaa kusikia baadhi ya watu wanasema kuwa baada ya kushindwa ubunge nimekimbia jimbo na kwenda Arusha, napende kuwaambia kuwa mimi bado nipo katika mji wa Kahama na ninaedelea biashara zangu katika mji huu”. Alisema Lembeli.
No comments: