LIVE STREAM ADS

Header Ads

LEMBELI AWATAHADHARISHA WAKAZI WA JIMBO LA KAHAMA MJINI KUHUSU VICHINJIO VYAO

Na:Shaban Njia
Mgombea Ubunge katika Jimbo jipya la Kahama mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA James Lembeli amewatahadharisha wakazi wa jimbo hilo wasihadaike na baadhi ya wafanyabiashara wanaonunua stashahada zao za kupigia kura.

Lembeli aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Cafe Latino kata ya Majengo Mjini Kahama na kubainisha kuwa kuna baadhi ya Wafanyabiashara wakubwa Wilayani Kaama wameamua kufanya mchezo mchafu wa kununua stashahada (VICHINJIO) ili kumnusuru mgombea Ubunge katika Jimbo hilo kupitia CCM Jumanne Kishimba ili apite kirahisi.

“Ndugu wananchi kuna mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya Wafanya biashara wa hapa Kahama wa kununua stashahada za kupigia kura kwa watu, nawaambia hivi imekula kwao na kwa taarifa yao nawajua na majina ninayo". Alisema Lembeli.

Kwa bupande wake mgombea Ubunge katika Jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Jumanne Kishimba alisema Lembeli wakati akiwa bungeni alishindwa kushughulikia matatizo ya wananchi hata kwa kutumia mfuko wa Jimbo ambapo matatizo sugu yapo katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama, ukosefu wa umeme wa uhakika pamoja na miundombu ya barabara.

No comments:

Powered by Blogger.