LIVE STREAM ADS

Header Ads

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ACHUKUA TAHADHARI.

Na:Shaban Njia
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji Kahama Underson Msumba amesema kuwa atalamizika kuhamishia shughuli za uhesabuji wa kura za Uchaguzi Mkuu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama kutokana na ofisi yake kuwa jirani na ofisi za vyama mbalimbali vya siasa.

Akiongea jana na Mwandishi wa Habari hizi Ofisini kwake, Msumba alisema kuwa kutokana na Ofisi yake kuzungukwa kwa wingi na Ofisi za vyama vya upinzani vya siasa ameona ni vyema shughuli zote na uhesabuji wa Kura katika uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na rais unaotarajiwa octoba 25 mwaka huu zifanyikia katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo kunaweza kuwa salama zaidi.

“Hapa katika ofisi yangu nimezungukwa kwa karibu na Ofisi za Vyama vya CHADEMA, NCCR Mageuzi pamoja na ACT kwa hiyo kwangu kunaweza kutokea jambo lolote na baadaye nikashindwa kufanya kazi ndio maana nimeona shughuli zote za uhesabuji wa kura pamoja na kutangaza matokeo zitafanyika katika ofisi ya kiongozi huyo.

Akizungumzia kuhusu hali ya maandalizi ya uchaguzi katika Jimbo Jipya la Kahama Mjini, Mkurugenzi huyo alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri ingawa bado kumekuwa na kasoro ndogo ndogo ambazo zinaweza kurekebishika na kuisha kabla ya kuchaguzi kuanza.

Alisema kuwa mpaka kufikia hivi sasa badhi ya vifaa vya upigaji wa kura tayari vimekwisha wasili  katika Vituo husika kama vile Madaftari ya kupigia kura, Fomu, Masanduku pamoja na Vifaa vingine ambavyo vitasadia katika kukamiklisha zoezi hilo la upigaji wa kura katika Jimbo zima la Kahama Mjini.

Alisema kuwa katika utaratibu aliouandaa wa kupiga hizo ni kuwa kutakuwa na mistari mitatu huku akiongeza kuwa mmoja utakuwa kwa ajili ya Wanaume, Mwingine kwa ajili ya Wanawake na wa Mwisho utakuwa kwa ajili ya makundi maalumu kama vile akina mama Wajawazito, watu Wenye ulemavu, wazee pamoja na watu wenye ualibino.

“Ninawataka Wananchi wakati wa kupiga kura kuzingatia taratibu pamoja na sheria na Uchaguzi utakuwa huru na wa haki kwa kila Mtanzania atakayekuwepo katika eneo la kupiga hali itakayonyesha uhuru na amani”. Alisema Msumba.

Akizungumzia hali ya Kampeni za Wagombea Udiwani na Ubunge katika maeneo yao, alisema kuwa hali ya Demokrasia bado ni ndogo na kuongeza kuwa Wagombea wengi wamekuwa wakitoa lugha za matusi kwa Wananchi badala ya kunadi sera zao ili Wananchi waweze kuchuja na kupata kiongozi atakayeweza kuwaongoza.

No comments:

Powered by Blogger.