LIVE STREAM ADS

Header Ads

LOWASA AWASHUKURU WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KWA MAHABA WALIYOMUONYESHA.

Umati wa wananchi na Makada waChama cha Maendeleo Chadema wakiwa katika Mkutano wa Mgombea Urais wa Chama hicho chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Chadema Mhe.Edward Ngoyai Lowasa uliofanyika hii leo katika Uwanja wa Furahisha Ilemela Mkoani Mwanza.

Katika Mkutano huo ambao umehudhuriwa na makada na viongozi mbalimbali wa Ukawa, Mhe.Lowasa amewashukuru wananchi kwa mwitikio wao mkubwa uliouta mahaba yaliyopitiliza ambapo amewaomba kuhakikisha wanawachagua viongozi wanaotokana na Ukawa kuanzia ngazi ya udiwani, Ubunge na Urais.

Amesema akipata ridhaa ya kuwa rais atahakikisha anapunguza kiwango cha umaskini nchini pamoja na kuboresha kiwango cha elimu pamoja na kuboresha ya wanchi kupitia makundi mbalimbali kama vile bodaboda na wengineo.
Umati wa wananchi na Makada waChama cha Maendeleo Chadema wakiwa katika Mkutano wa Mgombea Urais wa Chama hicho chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Chadema Mhe.Edward Ngoyai Lowasa uliofanyika hii leo katika Uwanja wa Furahisha Ilemela Mkoani Mwanza.
Mhe.Lowasa akiwahutubia wakazi wa Jiji la Mwanza hii leo katika Uwanja wa Furahisha
Mgombea Urais mwenza wa Ukawa Juma Duni Haji akiomba kura kwa wakazi wa Jiji la Mwanza hii leo katika Uwanja wa Furahisha
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Fredireck Sumaye akiwaombea kura wagombea wa Ukawa kwa wakazi wa Jiji la Mwanza hii leo katika Uwanja wa Furahisha
Aliekuwa kada wa CCM Kingunge Ngomare Mwilu alietimkia Team Mabadiliko akiwaombea kura wagombea wa Ukawa kwa wakazi wa Jiji la Mwanza hii leo katika Uwanja wa Furahisha
Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana (Chadema) Ezekiel Wenje
Wakifuatilia matukio kwa ukaribu zaidi
Hisia zilitawala
Ufuatiliaji kwa ukaribu zaidi
Ufuatiliaji mkutano wa Ukawa hii leo katika Uwanja wa Furahisha
Mabadiliko
Haya ni Mahaba Mazito
Team mahaba
Matukio yakifuatiliwa kwa Umakini zaidi
Ahadi zikifuatiliwa kwa umakini zaidi
Kila Kona
Kila Kona, wakifuatilia matukio
Mgombea Ubunge Viti Maalumu (Chadema) Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Wazee wa Matukio
Kinasa Matukio juu kwa juu
Citizen Tv kutoka nchini Kenya iliungana na vyombo vya habari nchini Tanzania kunasa matukio
Kutoka Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Mimi ni George Binagi-GB Pazzo.

No comments:

Powered by Blogger.