MGOMBEA URAIS MWENZA WA CCM ASIKITISHWA NA HUDUMA ZA AFYA WILAYANI KAHAMA.
Na:Shaban Njia
Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Hassan Suluhu amesema kuwa kwa sasa majengo ya hospitali ya Wilaya ya Kahama yanayotumika kuwahudumia wagonjwa yamegeuka kuwa nyumba za madaktari kwa kuwa wizara ya Afya na ustawi wa Jamii haipeleki dawa za kutosha.
Samia aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia wakazi wa Mji wa Kahama katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CDT mjini hapa, alipokuwa katika moja ya ziara zake zinazoendelea za kumnadi mgombea Urais Dr John Magufuli,wabunge na madiwani wanaotokana CCM.
Alisema ni ajabu haospitali zinakosa dawa lakini maduka ya Madawa yanayomilikiwa na wafanyakazi wa hospitali yanakuwa na dawa hali inayopelekea wagonjwa wote wanaokwenda kutibiwa hospitalini wanaandikiwa dawa nakwenda kununua nje ya hospiatali.
“Wananchi tafadhali chagueni CCM tunampango pekee wa kuboresha huduma ya Afya kwa jamii,ninyi mmekuwa mashahidi wazuri pindi mnapofika hospitalini kutibiwa mnaelezwa kuwa hospitali haina dawa lakini mnaandikiwa kununua nje ya hospitali,sasa hospitali ya kuaminika imegeuka kuwa maduka yao". Alisema Suluhu.
Alisema hospitali ya Wilaya ni hospitali inayopokea wagonjwa kutoka ndani na nje ya nchi, pia inapokea wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga haiwezekani kukosa dawa na waathirika wakubwa ni akina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano hivyo amepanga kukomesha hali hiyo iwapo CCM itaingia madarakani.
Katika mkutano huo aliwaomba wananchi hao kumchagua Jumanne Kishimba pamoja na madiwani wote wa chama cha Mapinduzi ili kusaidiana kukemea maovu sambamba na kuzidi kuleta maendeleo kwa wananchi wa Wilaya hiyo na kuongeza kuwa wasipomchagua Kishimba watakuwa wamemnyima Magufuli kutoa fursa ya maendeleo kwao.
No comments: