LIVE STREAM ADS

Header Ads

UONGOZI WA TOTO AFRICAN SPORTS CLUB YA JIJI MWANZA WAKAMILIKA.

Na:Oscar Mihayo
Hatimae uongozi wa Klabu Soka ya Toto African Sports Cluba ya Jiji Mwanza inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imefanikisha kupata uongozi mpya wa mwenyekiti na wajumbe wawili kupitia mkutano wake mkuu.

Awali timu hiyo ilikuwa ikiongozwa na makamu mwenyekiti tu ambae ni Waziri Gao kwa kipindi kirefu kabla ya kupata uongozi mpya hapo juzi katika ukumbi wa vizano hotel jijini Mwanza.

Akiwatangaza washindi, msimamizi  wa uchaguzi huo Ayoub Nyenzo kutoka Shirikisho la Soka nchini TFF, alisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki ambapo alimtangaza Godwin Aiko kuwa mwenyekiti wa timu hiyo baada ya kupata kura 37 dhidi ya Octavian Komba aliyepata kura 16 ambapo wanachama ya waliopiga kura walikuwa 54.  

Kwa upande wa wajumbe, washindi ni Timoth Kilumile aliyepata kura 52 na Lushinge Lushinge aliepata kura 23 ambapo sasa jopo la uongozi wa timu hiyo limekamilika na wameahidi kuifikisha mbali klabu hiyo kisoka.

Mkurugenzi wa wanachama wa (TFF) Eliud Mvera alisema kuwa umoja wa Toto umerudi na kuwataka kuunganisha nguvu zao kwa pamoja na kuweza kumaliza migogoro inayowakabiri huku akimtaka mwenyekiti mpya aliechaguliwa kuitisha kikao haraka iwezekanavyo ili kumaliza tatizo la taarifa ya utekelezaji wa shughuli za timu hiyo.

Licha ya kuwa wamepata uongozi mpya lakini hali bado si shwali katika klabu hiyo mara baada ya kocha mkuu wa Toto Martin Grelics kutishia kupeleka timu mazoezini ikiwa wachezaji hawatalipwa fedha wanazodai kiasi cha takribani shilingi milioni 12.

Grelics alisema fedha wanazodai wachezaji hao ni pamoja na fedha za usajiri, mishahara pamoja na posho za safari ya michezo ya nje ya mikoa.

No comments:

Powered by Blogger.