LIVE STREAM ADS

Header Ads

SAMIA SULUHU HASSAN; ELIMU BURE KUPUNGUZA MIMBA ZA UTOTONI KANDA YA ZIWA.

Na:Shaban Njia
Kauli ya Mgombea Urais Kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dtk.John Pombe Magufuli kuwa Serikali yake itakaposhika Dola itatoa Elimu bure kutoka Shule za awali hadi kidato cha nne, itasaidia kupunguza mimba za utotoni kwa Watoto wakike walio wengi kanda ya ziwa.

Mgombea Mweza wa Uraisi kwa tiketi ya Chama chama hicho Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo juzi katika Mkutano wa hadhara wakati akimwombea kura mgombea urais Urais Dkt.John Magufuli katika Viwanja vya CDT Wilayani Kahama.

Mgombea Mwenza huyo alisema kuwa kundi kubwa la Watoto wa kike wanapata ujauzito wakiwa na umri Mdogo ni kuanzia mika 13 hadi 15 amba wengi wao huwa majumbani baada ya kumaliza Elimu ya msingi na kusubiri kuolewa.

Alisema kuwa kutoka na matatizo hayo kama Wanachi watakichagua chama cha mapinduzi kwa awamu ya tano kiuongoza nchi watahakikisha kuwa ujenzi wa Mabweni kwa Wanafunzi wakike unafanyika ili kupunguza mimba nyingi za utotoni zisizokuwa za lazima.

Pia aliwataka Wazazi kuwapa kipaumbele Watoto wa kike katika suala zima la kuwatia Elimu kama wanavyowapa Watoto wa kiume  kwani suala la Elimu ni haki ya kila mtu na sii la mtu mmoja.

Mgombea Mwenza huyo alisema kuwa Wilaya ya Kahama inakabiliwa na Changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na masuala ya Afya, Barabara, pamoja na suala la umeme wa kudumua ambalo limekuwa ni kero kubwa kwa Wananchi wa Mji huo.

Katika suala la Bima ya Afya Mgombea huyo alisema Serikali yake imejipanga kuboresha huduma hasa katika usiamamiz endelevu wa dawa na kuongeza kuwa hata huduma zitaboreshwa ikiwa ni sambamba na kuongezwa kwa vifaa Tiba pamoja na wahudumu weledi.

Hata hivyo aliwataka Wananchi kuchangamkia huduma hiyo ya Bima ya Afya ili kupunguza msongamano wa Wagonjwa Hospitalini hali ambayo itachangia Wagonjwa kupata huduma kwa urahisi  kupata matibabu kwa haraka tofauti na hapo awali.

Awali akiongea kabla ya kumkaribisha Mgombea Mwenza, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM) Christopher Ole Sendeka alisema Mbunge aliyekuwapo katika kipindi cha nyuma katika Jimbo la Kahama James Lembeli alimua kuhama CCM Mwenyewe na hakufukuzwa na mtu yeyote kama anavyodai.

“Hakuna mtu pale Bungeni alikuwa rafiki yangu kama aliyekuwa Mbunge wenu kipindi kichopita James Lembeli, Lembeli aliwalaghai Watanzania  na hatimaye baadaye akaamua kujiumbua mwenyewe kwa Kuhamia Chadema". Alisema Ole Sendeka.

No comments:

Powered by Blogger.