LIVE STREAM ADS

Header Ads

MGOMBEA UBUNGE ACT WAZALENDO JIMBO LA MUHAMBWE MKOANI KIGOMA AWAAHIDI NEEMA WAKULIMA.

Na:Shaban Njia
Mgombea Ubunge kupitia chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo la Muhambwe lililopo Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma Edger Mkosamali amesema kuwa iwapo kama atapata ridhaa ya kuwaongoza Wananchi wa Jimbo hilo atahakikisha kuwa soko la uhakika la Mhogo linapatikana jimboni humo

Mkosamali aliyasema hayo katika Mikutano yake katika Vijiji vya Kagezi, Busunzu, Bunyambo, Kibuye, Kichanonga pamoja na Mabamba alipokuwa katika ziara ya kunadi sera zake kwa Wananchi kuhusu ahadi alizojiwekea kuzitekeleza pindi atakapopata fursa ya kuwa mbunge.

Alisema kuwa kwa sasa katika jimbo hilo Wananchi wamekuwa wakiuza zao hilo kwa bei ndogo hali ambayo imefanya Wananuzi wengi kutoka katika nchi jirani ya Burundi kununua zao hilo na kusafirisha nchini kwao .

Alisema kwa sasa ni budi kwa Wananchi wa Jimbo hilo kuanzisha vyama vya Msingi kwa Wakulima wa zao la Mhogo ambali linalimwa kwa Wingi katika Jimbo hilo na hivyo kupelekea kuwa rahisi kupata mikopo itakayoimarisha Mitaji yao.

“Kutokana na Wingi wa Wakulima wa Mhogo katika Jimbo langu pia nimeazimia kujenga soko la Kimataifa katika Kata ya Busunzu na pia inunuliwe kwa dola kwani wafanyabiasha wengi wa zao hilo wanatoka katika nchi za Burundi na Rwanda”. Alisema Mkosamali.

Pia aliahidi kujenga kiwanda cha sukari katika jimbo hilo kwani kuna maeneo yanayofaa kwa kilimo cha Miwa ikiwa kama kama yeye pamoja na wagombea ubunge wengine wanane wa ACT Wazalendo Mkoa wa Kigoma (Timu Mawese) watachaguliwa.

Nae Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe alisema kuwa kwa Nchi ya Tanzania inazalisha kiasi cha tani 350,000 za Sukari huku mahitaji ya Watanzania uzalishaji wa Tani 500,000 hali ambayo inasababisha upungufu mkubwa Sukari na kufanya Serikali kununua bidhaa katika nchi za Malaysia kiasi cha tani 150,000.

Aidha alisema kuwa Kama Mkoa wa Kigoma ukifanikiwa kupata Kiwanda cha Sukari unaweza kuzalisha kiasi cha tani 100,000 kwa mwaka na hivyo kupelekea kupunguza tatizo hilo kubwa liliopo hapa nchini.

“Tuna Bonde la Mto Malagarasi, lenye ukubwa wa Hekta100,000 linalofaa kwa Kilimo cha Miwa na Mwekezaji atakayepatikana atapewa kiasi cha Hekta 30,000 tuu  na zilizobaki 70,000 watapewa Wakulima kwa ajili ya kuanzisha mashamba yao ya Miwa watakayouza katika Kiwanda hicho. Alisema Kabwe.

No comments:

Powered by Blogger.