LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHEREHE ZA HARUSI MKOANI SHINYANGA MARUFUKU ILI KUTOKOMEZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU.

Na:Shaban Njia
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Ntuzu Kapologwe amepiga marufuku Sherehe za harusi zinazofanyika Mkoani Shinyanga, kwa lengo la kuondoa kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu uliozuka hivi karibuni katika Mkoa huo.

Kapologwe alitoa onyo hilo wakati akizungumza katika kikao baina ya Waandishi  wa habari na Mfuko wa  Bima wa Afya (NHIF) uliofanyika mjini Shinyanga kwa lengo la kuwahamashisha Waandishi wa habari kujiunga na ufuko huo.

Kaporogwe alisema kuwa ugonjwa wa kipindupindu tayari umeshaingia katika Mkoa wa Shinyanga na tayari wagonjwa nane wameishagundulika kuwa na vimelea vya ugonjwa huo katika Wilaya za Kishapu, Shinyanga na Kahama.

Alisema kuwa kutoka na ugonjwa huo kugundulika katika Mkoa wa Shinyanga Wananchi wanatakiwa kwa sasa kuzingatia suala la usafi na kuepuka kula vitu ambavyo sio vya moto kwa lengo la kuepuka kuendelea kusambaa kwa ugonjwa huoa katika Mkoa wa Shinyanga.

Aidha alisema baadhi ya Wagonjwa hao wanatoka eneo la Mhongolo Wilayani Kahama, Kishapu, Simiyu pamoja na manispaa ya Shinyanga hali ambayo inatishia kunea kwa kwa kasi kwa ugonjwa huo ambao umezinduka hivi karibunio katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mgamnga Mkuu huyo aliwataka Wasafiri wanaosafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kutojihusisha na ulaji wa Vyakula mbalimbali wawapo njiani hali ambayo inaweza kuwa moja ya changamoto ya kupunguza muenea kwa ugonjwa huio kwa haraka katika Mkoa wa Shinyanga..

Pamoja na Mambo mengine katika Kikao hicho baina ya Waandishi wa Habari Meneja Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Shinyanga Emmanuely Amaniu alisema kuwa Mfuko huo umeona ni mhimu kwa kundi la waandishi wa Habari kwa sasa kuingia mpango huo wa Bima ya afya kwani kundi ambalo linatoa Elimu kwa jamii.

Alisema kuwa Mfuko huo unatoa mafao 11 kwa wanachama wake na pia unasaidia katika kuepusha kuomba misaada mara kwa mara pindi matatizo yanapotokea kama vile ya misiba na mambo mengine ya kijamii.

Aidha alisema kuwa Mfuko huo unahusisha vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa kama vile vilabu vya Waandishi wa habari ambavyo vimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa jamii inapata ujumber kuhusu  masuala mazima ya Bima ya Afya.

Pia alisema kuwa baadhi ya Mkundi mangine ambayo yanaweza kupata msaada wa kujiunga na Bima ya Afya ni kama vile mama lishe , Bodaboda ambao tayari wameishajiunga katika vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali hali ambayo inaweza kuwakwamua kiuchumu na kuondoka na janga la umasikini.

Aman alisema kuwa Mfuko pia unatoa mikopo kwa Hospitali za Serikali kwa ajili ya kununua Vifaa tiba, madawa na fedha kwa ajili ya ukarabati wa Majengo katika Hospitali mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza huduma za Afya hapa nchini.
mwisho.

No comments:

Powered by Blogger.