LIVE STREAM ADS

Header Ads

MISUNGWI WA CHADEMA AWAAHIDI MAZIWA NA ASALI WANANCHI WA KATA YA BUKANDWE MAGU.

Judith Ferdinand
Wananchi wa Kijiji cha Iyabuyaga kilichopo katika Kata ya Bukandwe Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, wameahidiwa kutatuliwa changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo tatizo la maji linayowakabili kwa miaka mingi, elimu pamoja na ajira kwa vijana.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na mgombea udiwani katika Kata hiyo, kupitia Chama  Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Willyfred Misungwi kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika katika uwanja wa kijiji cha Iyabuyaga Wilayani humo.

Alisema wananchi wanashindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali hasa wakati wa kiangazi, kwani hulazimika kutembea zaidi ya kilomita mbili kufuata majivhali inayopelekea kushuka kwa uchumi binafsi na taifa.

Pia alisema kata ya Bukandwe inahitaji million 120, kwa ajili ya maji na endapo kama atapatiwa ridhaa ya kuongoza kata hiyo, atashirikiana na wananchi wake ili kutatua changamoto hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.

Misungwi alisema kuwa endapo kama mpango huo utashindikana, ataandika mradi na kuupeleka halmashauri kwa ajili ya kuomba fedha ili katika kipindi cha bajeti ya mwaka 2016/2017, halmashauri iweze kutenga pesa hizo kwa ajili ya maendeleo ya maji katika kata hiyo.

Hata hivyo alisema kuwa mambo mengine atakayoyapa kipaumbele ikiwa kama atafanikiwa kushinda katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba 25 mwaka huu, ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora, kwa kuboresha mazingira na vitendea kazi.

Aidha alisema kuwa mambo mengine atakayosimamia ni ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuanzisha taasisi kwa ajili ya kuwaunganisha wawekezaji ili kutengeneza mfumo wa ustawi wa jamii ndani ya kata hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.