LIVE STREAM ADS

Header Ads

SEHEMU YA SITA: HATUA SITA MUHIMU MTU ANAZOTAKIWA KUPITIA ILI KUFANIKIWA.

Soma HAPA Sehemu ya Tano
HATUA YA SITA NI MAFANIKIO (SUCCESS).
Jihn Rohn once said that success is like ocean, but most people took spoons to carry water when they comes to ocean, Yaani mafanikio ni kama bahari lakini tatizo la watu wengi hubeba vijiko pindi wanayafuata mafanikio. 
Hii ndio sababu kubwa watu wengi wanaishia kuishi maisha duni na ya kawaida sana na na hawapati kile ambacho wanakihitaji katika maisha yao.
Mafanikio ni matokeo ya kufanya mambo madogo madogo kila siku kwa umakini wa hali ya juu na kujituma pasipo kukoma wala kukata tamaa, watu wote waliofanikiwa wanafanya kazi kwa bidii nikisema kwa bidii ninamaanisha wanajituma na wanatumia maarifa katika kufanya kazi zao, wewe kama unafikiri kufanikiwa ni kufanya kazi ngumu nakupa pole maana ingekuwa ni hivyo basi watu wanaopasua kokoto, wabeba matofali, na wanaofanya kazi za aina hiyo wangekuwa ndio wamefanikiwa.
Pindi unapofikia hatua hii ya mafanikio hutakiwi kuridhika na kusema basi sitakiwi kujituma tena bali unatakiwa kuendelea na kazi zako kama kawaida na kuwa nidhamu katika shughuli zako. Fedha ina tabia ya kumkimbia mtu ambaye anaridhika mapema na asiyekuwa na nidhamu katika matumizi yake.
Mafanikio hayaji kwa kuvunja sheria huja kwa kufuata sheria na kuzitendea kazi kwa mfano kuna sheria ambayo inatawala kiasi cha fedha ambacho mtu anakuwa nacho nayo inasema kiasi cha fedha ambacho mtu anakuwa nacho kinakuwa sawa sawa na.
1.Uhitaji wa kitu ambacho mtu anafanya, kama jambo ambalo unafanya jamii yako ina uhitaji mkubwa nalo inamaanisha kwamba watu watatumia na kununua kwa kiasi kikubwa kile kitu unachouza au huduma fulani ambayo unatoa nawe utapata mafanikio makubwa. 
Hebu tujiulize kama Barkresa, Mohamed Ent na Dr. Mengi bidhaa zao watu wangekuwa hawazihitaji ingekuwaje? Ni dhahiri wasingezinunua wala kuzitumia hivyo wasingeweza kufanikiwa. 
Njia pekee iliyomfanya Bill Gates kuwa tajiri namba moja duniani ni kwa kuuza programu ambazo kila mtu anauhitaji nazo hivo kwa sababu hiyo imesababisha yeye kujikusanyia mabilioni ya dola jana nlikuwa nasoma habari za Bill Gates kulingana na utajiri wake anaweza kumgawia kila mtu duniani $15 sawa na Tshs 32,467.53 na bado akabakiwa na utajiri wa $15millioni.
2.Uwezo wako katika kufanya kitu fulani, kama unaweza kufanya kitu kwa ufanisi wa hali ya juu basi jua uwezekano wako wa kufanikiwa unaongezeka zaidi hebu angalia mpiganaji ndondi maarufu duniani ambaye ametangaza kutopigana tena duni Floyd Mayweather anaepigana mara moja tu au mara mbili kwa mwaka kwa dakika 33/64 lakini analipwa mamilioni ya pesa kutokana na uwezo wake tu wa kupigana hivyo basi kama wewe ni muimbaji,muigizaji, mtangazaji, na kadhalika basi uwezekano wako kufanikiwa sana upo kama utasaka maarifa ya kutosha katika kitu unachokifanya na kuyatendea kazi.
3.Ugumu wa kupata mtu wa kukaimu nafasi yako, kama kitu unachokifanya ni vigumu kupata mtu mwingine wa kukifanya kama wewe basi ni lazima utafanikiwa maana utakuwa ni wewe mwenyewe unaweza kukifanya na hamna wa kufanya namna unavyofanya hivyo kama ni sokoni basi utaweka bei ambayo unataka wewe maadamu hauna mshindani, hii itakusaidia kuzidi kufanikiwa katika unachokifanya kwa hali ya juu zaidi.
Ili kufanikiwa zaidi katika maisha ni dhahiri kwamba unatakiwa kuwa na malengo kwenye maisha yako na haya malengo ndio yanakupa mwanga unatakiwa kufanya nini na utafanyaje ndipo utapata mafanikio, usiishi kwa kubahatisha na kusema bora siku imepita kuwa na misimamo yako jua kabisa unataka nini kwenye maisha yako na kuwa na mpango wako madhubuti wa kupata hicho ambacho unakitaka.
Mafanikio makubwa hayaji kwa kuwa na ndoto za kuhudumia watu wachache yanakuja kwa kuwa na ndoto za kuhudumia mamilioni ya watu. Sasa usiwe na mawazo mafupi ya kuwahudumia watu ishirini kwenye mtaa wenu kwa hilo duka lako uliloanzisha na ukawa na mategemeo ya kuwa na mafanikio makubwa. Sio kwamba nadharau mwanzo mdogo La hasha! ninadharau mwanzo mdogo usioendelea kama leo kulingana na bajeti yako unaweza kuhudumia watu ishirini basi baada ya miezi mitatu au sita uwe na mpango wa kuweza kuhudumia watu 150-300 kwa siku na baada ya mwaka waongezeke miaka waongezeke maradufu.
Nataka nizidi kukukumbusha adui wa kwanza wa mafanikio yako ni wewe peke yako, Rose Muhando ana wimbo ambao unaitwa umejiloga mwenyewe, kwa nini anasema ivo ni kwa sababu anaefikiri, anaeamua, anaetenda ni wewe na sio mwingine yeyote kwa hivyo wewe kukaa na kulalamikia hali fulani ambayo unapitia kwamba ndio inasababisha usifanikiwe sio sahihi kabisa na unatakiwa kubadilika.
Hii ndio maana George Bernad Show alisema ''People are always blaming circumstance for what they are, i don't believe in circumstance the people who make on this world are the people who go and look for circumstance that they want if they cant find them they make them" kama hupendi hali fulani unayopitia kimaisha basi jua una uwezo wa kuibadilisha na jua kabisaa hakuna mtu mwingine wa kuibadilisha isipokuwa wewe.
Watu waliofanikiwa kulingana na Bernad Show ni wale waliotoka na kwenda kutafuta hali za maisha wanazozitaka na kama hawakuzipata basi walizitengeneza je wewe unataka nini maishani mwako na umefanya nini na kuchukua hatua zipi kuhakikisha unapata hicho unachokitaka? Ubaya huwa watu wengi huwa hawachukui hatua wanabaki kulalamika na wanasahau kwamba mwenye uwezo wa kubadili maisha yao ni wao wenyewe sio Serikali.
MWISHO
IMEANDALIWA NA LIFE SECRETS COMPANY-MWANZA.

No comments:

Powered by Blogger.