LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MKUU WATAKIWA KUTENDA HAKI.

Na:Shaban Njia
Wasimamizi wa uchaguzi mkuu katika halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutokuingiza itikadi zao za kisiasa katika zoezi hilo kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria ya uchaguzi hali ambayo inaweza kusababisha vurugu zitakazohatarisha amani.

Hayo yalisema juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kahama ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilayani humo Benson Mpesya katika mafunzo kwa wasimamizi wa kata watakaosimamia zoezi la uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika octoba 25 mwaka huu.

Mpesya alisema kuwa kuna baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi wababaishaji ambao huingiza itikadi zao zakisiasa kwa kushirikiana na mawakala wa vyama na kuvuruga uchaguzi hadikupelekea kuibuka kwa fujo kutoka kwa wananchi baada ya matokeo kutangazwa.

Hata hivyo Mpesya aliwasihi wasimamizi kusimamia majukumu yao kikamilifu licha ya kuwepo kwa kauli mbalimbali zinazotolewa katika majukwaa ya kampeni za siasa kwani hakuna dira ya mabadiliko ya Taifa kama uchaguzi hivyo ni vyema wakalizingatia hilo wakati wa uchaguzi.

“Kumekuwa na wasimamizi ambao wamekuwa na ushabiki wa kisiasa hasa wakati wa uchaguzi ambapo wamekuwa wakitoa maneno ambayo sio rafiki kwa wananchi na wakati mwingine wamekuwa hata wakiwalazimisha wananchi kumchagua mtu wanaemtaka wao, hivyo basi kwa yule atakaebainika sheria itachukua mkondo dhidi yake". Alisema Mpesya

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba alisema kuwa wao kama wasimamizi wakuu wa uchaguzi wamejipanga kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu utazingatia demokrasia kwa kuzingatia usawa bila kupendelea chama chochote.

Alisema kuwa kufuatiwa na sheria mabazo zimewekwa kwa mawakala wa usimamizi wa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu,sheria hizo zinawabana wasimamizi kutokupendelea ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na masuala ya kisiasa.

“Mimi nawaomba sana wasimamizi wa uchaguzi huu tutende haki na usawa bila kupendelea chama chochote kwani tukifanya hivyo tutakuwa tunakiuka sheria ya usimamizi wa uchaguzi na inaweza kutuletea vurugu na wakati mwingine kuleta maafa kwa watanzania wasio kuwa na hatia”. Alisema Msumba.

No comments:

Powered by Blogger.