LIVE STREAM ADS

Header Ads

ALLIANCE WAANZA VEMA MICHUANO YA LIGI DARAJA LA PILI TAIFA.

Timu ya Soka ya Alliance Sports Academy ya Jijini Mwanza imeianza vema Michuano ya Ligi Daraja la Pili ngazi ya Taifa baada ya kuitandika timu ya Madini ya Mkoani Arusha kwa bao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa CCM Kirumba.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Bao la kwanza la Alliance lilifungwa na Athanas Mdamu dakika ya 32 kipindi cha kwanza huku la pili likitiwa kimiani na Martin Kiggi kunako dakika ya 89 kipindi cha pili ambapo Alliance wamejiweka katika wakati mzuri pindi watakaporudiana na timu hiyo ya Madini.
Kikosi cha Timu ya Alliance Sports Academy ya Jijini Mwanza kinachoshiriki Ligi Daraja la Pili Taifa
Kikosi cha Timu ya Madini Fc ya Mkoani Arusha kinachoshiriki Ligi Daraja la Pili Taifa
Waamuzi wa mechi na Makeptaini wa timu
Mwamuzi wakirusha shilingi juu
Mlinda mlango wa Alliance akiongoa mpira katika lango lake
Mlinzi wa Timu ya Madini akipambana kumzuia mshambuliaji wa Alliance ili asiweze kufanya shambulizi katika lango la timu yake
Wachezaji wa Alliance wakishangilia baada ya kufunga bao
Washangiliaji wa Alliance wakishangilia ushindi huku wakiwa na ngoma ya Ritungu kutoka Mkoani Mara
Mashabiki wa Alliance wakishuhudia mtanange baina ya timu hiyo na Madini kutoka Mkoani Arusha
Kutoka Kushoto ni Waziri Gao Makamu, Mwenyekiti wa Timu ya Toto, Jackson Songora, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mwanza MZFA na John Tegete Kocha Msaidizi timu ya Toto wakishuhudia mtanange baina ya Alliance na Madini
Mchezo huo ulikuwa ukirushwa moja kwa moja na Afya Radio ya Jijini Mwanza
Kocha Mkuu wa Alliance Mohamed Tajdin akizungumzia mchezo huo
Kocha Msaidizi wa Alliance, Mathias Wandiba akizungumzia Mchezo huo
Kutoka Uwanja wa CCM Kirumba, Mimi ni GB Pazzo (Kulia) nikiwa na mwanahabari nguri wa habari za Michezo Jijini Mwanza Mariam Juma (Kushoto)

No comments:

Powered by Blogger.