LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBIO ZA ROCK CITY MARATHON 2015, WAKENYA WAFANYA KWELI.

Washiriki wa mbio za Rock City Marathon 2015 kwa Km.21 wakianza kutimua mbio hizo jana katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Katika mbio hizo Washiriki kutoka nchini Kenya waliibuka kidedea kwa kunyakua nafasi ya kwanza kwa wanawake na wanaume ambapo kwa Wanaume Mshindi ni Festus Taram kutoka Kenya Saa 01:04:40, Mshindi wa Pili Evancy Kiplagan kutoka Kenya saa 01:04:55 na mshindi wa tatu ni Fabian Joseph kutoka Arusha Tanzania alietumia saa 01:05:00.

Kwa upande wa Wanawake Km 21, Mshindi ni Alice Mogire kutoka Kenya saa 01:14:42, wa pili ni Natalia Elisante alietumia muda wa saa 01:15:16 na wa tatu ni Angelina Tsere alietumia saa 01:15:35 ambapo wote wawili wanatokea Arusha Tanzania.

Mshindi wa Kwanza katika mbio hizo za Km 21 alijinyakulia kitita cha shilingi Tsh.1,500,000 wa pili Tsh.900,000 wa tatu Tsh.700,000 wa nne na wa tano Tsh.100,000 na wa sita hadi wa kumi Tsh.50,000

Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International na kudhaminiwa na Makampuni mbalimbali ikiwemo Mdhamini Mkuu Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF, Precision Air, Bodi ya Utalii Tanzania, New Mwanza Hotel na Bank M ambapo lengo lake ni kukuza mchezo wa riadha pamoja na kuhimiza utalii wa ndani.
Washiriki wa mbio za Rock City Marathon 2015 kwa Km. 5 wakianza kutimua mbio hizo jana katika Uwanja wa Mabatini
Washiriki wa mbio za Rock City Marathon 2015 wakikata upepo katikati ya Jiji la Mwanza zilipofanyikia mbio hizo
Silas Lucas Nyalali ambae ni Mwenyekiti wa Riadha Mkoa wa Mwanza akitoa ufafanuzi kwa Washiriki wa mbio za Rock City Marathon 2015 kabla ya kuanza mbio hizo jana Jijini Mwanza
Peter Mwita ambae ni Mjumbe wa Chama cha Riadha Taifa akitoa ufafanuzi kwa Washiriki wa mbio za Rock City Marathon 2015 kabla ya kuanza mbio hizo jana Jijini Mwanza
Mshindi wa Kwanza wa Km 21 wanaume Festus Taram akipokea zawadi yake
Katikati ni Mshindi wa Kwanza Mbio za Rock City Marathon 2015 Festus Taram (Kenya), Kushoto ni Mshindi wa Pili Evancy Kiplagan (Kenya) na Kulia ni Mshindi wa tatu Fabian Joseph (Tanzania)
Mshindi wa Kwanza wa Mbio za Rock City Marathon 2015 Km 21 Wanawake Alice Mogire (Kenya) akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi Willium James ambae ni Afisa Michezo Mkoa wa Mwanza (Akimwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza).
Kutoka Kulia ni Natalia Elisant,e Mshindi wa Pili Km 21 Wanawake (Arusha Tanzania), Alice Mogire, Mshindi wa Kwanza Km 21 Wanawake (Kenya) na Angelina Tsere, Mshindi wa tatu Km 21 Wanawake kutoka Arusha Tanzania.
Iren Fidelis kutoka Jijini Mwanza akipokea nishani yake kutoka kwa mgeni rasmi baada ya kuibuka Mshindi wa Kwanza Km 2 Watoto upande wa Wasichana.
Katika Mbio hizi Mshindi wa Kwanza alijinyakulia Tsh.30,000 wa pili Tsh.20,000 wa Tatu Tsh.15,000 na wa nne hadi wa kumi Tsh.5,000
Washindi wa Mbio za Rock City Marathon Km 2 Watoto upande wa Wasichana ambapo Katikati ni Mshindi wa Kwanza Irene Fidelis, Kushoto ni Esther Mashaka Mshindi wa pili na Kulia ni Suzan Vedastus ambae ni Mshindi wa Tatu, Wote wanatoka Jijini Mwanza
Washindi wa Mbio za Rock City Marathon Km 2 Watoto upande wa Wavulana ambapo Katikati ni Simon James, Kushoto ni Simon Ngwata, Mshindi wa Pili na wote wanatokea Nyamohongolo Jijini Mwanza ambapo kulia ni Edison Alex ambae ni Mshindi wa tatu akitokea AICT Ilemela.
Nindilo Yusto ambae ni Mshindi wa Kwanza na wa pekee katika mbio za Km 3 Wazee kwa upande wa Wanaume
Washindi wa Mbio za Km 3 Wazee kwa Upande wa Wanawake ambapo Mshindi wa kwanza ni Christina Urio (Kulia) na mshindi wa pili akiwa ni Tatu Buta (Kushoto) wote wakitoka Jijini Mwaza
Washindi wa mbio za Rock City Marathon 2015 kwa upande wa watu wenye alibinism ambapo Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Yohana Charles Mzela, Kushoto ni Mshindi wa Pili, Paschal Emmanuel Fidelis wote wakitoka Jijini Mwanza na Kulia ni Mshindi wa Pili, Benard Simika Kutoka Mkoani Geita
Washindi wa Mbio za Rock City Marathon 2015
Washindi wa Mbio za Rock City Marathon 2015
NSSF Mwanza pia walishiriki mbio za Rock City Marathon 2015
NSSF Mwanza pia walishiriki mbio za Rock City Marathon 2015
Kulia ni Mkimbiaji wa siku nyingi nchini Juma Maziku 

No comments:

Powered by Blogger.