LIVE STREAM ADS

Header Ads

WALIOOKOLEWA KATIKA MACHIMBO YA DHAHABU MKOANI SHINYANGA WAELEZA MAKUBWA.

Picha Kutoka Maktaba
Na:Shaban Njia, Kahama
WATU watano ambao ni Wachimbaji wadogowadogo katika Mgodi wa Nyangata Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameokolewa na wenzao baada ya kufukiwa na kifusi cha Udongo na kukaa kwa muda wa siku 41 bila ya kula kitu chochote.

Wakiongea na Waandishi wa Habari wakiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama walipolazwa,Wachimbaji hao walisema kuwa walikuwa katika shimo hilo kwa siku hizo huku wakiwa wakila mizizi  huku wakitumia kofia zao katika kukinga maji yaliokuwa yakitiririka kutoka juu kwa ajili ya kunywa .

Mmoja wa Wachimbaji hao  Chacha Wambura, Alisema kuwa katika shimo hilo walikuwa jumla ya wachimbaji sita waliofukiwa lakini mmoja wao Musa Spana alifariki Dunia baada ya kukataa kula mizizi hali ambayo ilisababisha kupata Ugonjwa wa kuhara uliosababisha kifo chake.

“Tulikuwa tukitumia miti inayojengea  Mashimo (Matimba) kama chakula pamoja na wadudu wadogowadogo jamii ya mende na vyura ambapo maji tulikuwa tukitumia kofia zetu ( Helmet) kukinga maji yaliokuwa yakitoka juu ingawa yalikuwa ni machafu lakini mwenzetu mmoja Musa Spana alifariki baada ya kukataa kutumia vitu hivyo”, Alisema Wambura.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Madini Nchini Ali Samaje aliwataka Wachimbaji wadogowadogo kuimarisha Migodi huku wakizingatia masuala ya kiusalama zaidi hali ambayo itawafanya wachimbaji hao kufanya kazi zao kwa uhakika na kuepuka na ajali kama hizo.

Pia Kamishna huyo aliwataka pia kuacha kuchimba Madini kwa ajili ya kuuza tuu na kuongeza kuwa wajaribu saidizana katika mambo mbalimbali pindi wanapokuwa na matatizo kwani shughuli zao zipo wanazienesha katika maeneo ambayo hayapo salama.

Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Joseph Ngowi, alisema kuwa ameshtushwa na tuki hilo la Wachimbaji hao kukaa kwa muda huo katika shimo na kuongeza kuwa tukio hilo linawweza kuwa ni maajabu ya nane ya Dunia.

Dr, Ngowi aliwataja waliwataja Wahanga hao walionusurika katika kifo katika ajali hiyo kuwa Chacha Wambura, Amos Muhangwa, Joseph Burulwa, Msafiri Gerald , Wonyiwa Moris pamoja na Musa Spana ambaye alifariki dunia akiwa Shimoni.

Alisema kuwa kwa Wahanga hao wapo katika Hospitali yake chini ya usimamizi wa kitengo cha Lishe na saikolojia ili kuhakikisha kuwa wanarudi katika hali zao za kawaida kwa muda usiopungua siku saba.

“Wahanga hao tunao katika Hospitali yetu chini ya kitengo cha Lishe kwa kuwa hawaoni kwa muda huu mpaka muda wa siku saba upite kwani sehemu waliokuwepo palikuwa ni giza hali ambayo kwa sasa bado macho yao sio mazuri ikiwa ni sambamba na akili zao sio nzuri.

Pia alisema kuwa kutokana na kukaa shimoni kwa muda mrefu hali zao zimekuwa ni dhoofu na utumbo bado haujawa vizuri kwa hiyo kwa kuwatumia wataalamu wetu wa idara ya lishe kwa sasa tunawatengenezea chakula laini kama vile uji ili waweze kupata nguvu hali hiyo ya udhoofu itatoweka kwa muda wa siku saba kuanzia sasa.

No comments:

Powered by Blogger.