LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATU WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI JIJINI MWANZA KWA UTAPELI WA MTANDAONI.

Kutoka Kushoto ni Watuhumiwa Watatu wa Makosa ya Utapeli wa Mtandaoni wakifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Mwanza hii leo kwa ajili ya kusomewa mashtaka ya Utapeli wa Mtandaoni kujipatia pesa kutoka kwa wafanyabiashara kinyume cha sheria.
Na:Binagi Media Group
Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la kughushi nya nyaraka na kusajili lini za simu na kufungua akaunti za benki kwa majina ya vyama vya siasa vya Chadema na CCM na hivyo kuzitumia kuomba pesa kwa wafanyabiashara kwa ajili ya kuwasaidia kuendeshea shughuli za kampeni za uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni, huku wakiwaahidi wafanyabiashara hao kuwa watawasaidia (watawabeba) kwenye biashara zao uchaguzi ukimamilika.

Majina yao ni Boni Bukulu Tefe (40), Spridon Mutangalwa Njunwa (38) na Braiton Bugenyi Wilson (43) wote wakiwa ni wafanyabiashara na wakazi wa Jiji la Mwanza. Watarudishwa tena mahakamani Novemba 30 mwaka huu.

Mwanasheria Mwandamizi Mkuu, Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Johanes Kalungula ameseka watuhumiwa hao walifungua akaunti mbili feki katika benki ya NBM Tawi la Mwanza kwa majina ya M4C ya Chadema na CCM na kuana kuomba pesa kwa wafanyabiashara ambapo walifanikiwa kutapeli kiasi cha shilingi Milioni nne kabla ya kutiwa mbaloni.
Watuhumiwa wakisubiri kusomewa mashtaka yanayowakabiri
Mwanasheria Mwandamizi Mkuu, Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Johanes Kalungula akiongea na wanahabari nje ya mahakama ambapo amewasihi wananchi kuwa makini ili kupuka utapeli wa mitandaoni kwani watuhumiwa hao walikuwa wakituma msg za kuomba pesa kupitia laini za simu walizosajili kwa majina ya kughushi. Ameongeza kuwa serikali iko makini katika kupambana na utapeli wa kimtandao.

No comments:

Powered by Blogger.