LIVE STREAM ADS

Header Ads

HAYA NI MAAJABU. WAKAZI WA MJI WA KAHAMA WAOMBA BOMOABOMOA IHAMIE KATIKA MJI HUO.

Na:Shaban Njia, Kahama
Wakazi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga  wameitaka Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuhamishia  zoezi la bomoabomoa  Wilayani hapa  kutokana na baadhi ya wananchi kuvamia na kujenga  katika maeneo ya wazi  pamoja  na yale ya huduma za  jamii.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wanaoishi mjini  hapa  wameitaka serikali kupitia halmashauri ya mji wa Kahama kuendesha zoezi la bomoabomoa  kwa wale wote waliovamia na kujenga kwenye maeneo hayo.

Kajolo Mohami anayeishi mtaa wa Nyasubi  alisema  karibu maeneo yote ya wazi na yale ya huduma za jamii  mjini hapa yalishavamiwa na kujengwa na watu wenye fedha hali iliyosababisha  kuharibu taswira ya mpango miji.

Alisema  anapenda serikali kupitia halmashauri ya mji wa Kahama kuendesha zoezi hilo kama inavyofanyika Jijijini Dar-es-Salaam  kwa wale wote waliokuwa wamevamia na kujenga  kinyume cha sheria katika maeneo ya wazi.

Nae Peter Samson mkazi wa Majengo mjini alisema agependa  kuona bomoabomoa kama inayofanywa na jijini Dar na serikali  inafanyika mjini Kahama kutokana na kuwa maeneo  yote  ya wazi ya huduma za jamii , shule za msingi  watu walishayavamia na kujenga.

“Tunapenda kuona zoezi hilo linahamia katika mjui wa Kahama kwani kuna baadhi ya maeneo mengi yamevamiwa na wafanyabiasha wenye fedha na kuwekeza katika ujenzi wa mashule pamoja na ujenzi wa majumba katika maeneo zinapopita barabara hali amabyo imekuwa ni kero kwa Wananchi”. Alisema Samson.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba, aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa mji wa Kahama hauwezi kuendelea na kupata hadhi ya Manispaa bila ya kufanya zoezi la bomobomoa katika baadhi ya maeneo na mitaa yaliyojengwa kinyume cha sheria.

No comments:

Powered by Blogger.