LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAHAMA WAMWOMBA MAGUFULI KUYAONDOA MADUKA YA DAWA MHIMU YALIYOPO JIRANI NA HOSPITALI.

Na:Shaban Njia
WANANCHI wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wamemwomba Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa anayotoa maduka ya Dawa yaliopo jirani na Hospitali ya Wilaya, kwa lengo wagonjwa kupata huduma stahiki katika Hospitali hiyo badala ya Madaktari kuwaambia waende kupata huduma katika zahanati binafsi zilizopo katika eneo hilo.

Jana Wananchi hao walisema kuwa kwa kasi alioanza nayo Rais huyo awamu ya tano hasa katika Sekta ya Afya, ni bora  akayaondoa maduka maduka hayo ya dawa katika sehemu hiyo ili kuweza kuwasaidia wananchi wa hali ya chini ambao hawana kipato kikubwa katika kumudu gharama.

“Mimi ninashangaa ukienda katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kutafuta huduma za vipimo utaambiwa na Daktari nenda katika zahanati fulani ambapo huduma hiyo inapatikana, na ukifika katika Zahanati hiyo utamkuta Dackari huyo huyo ambaye alikwambia ukapime hivyo unapatwa na mstuko kujua kama anafanya kazi mbili katika maeneo tofautitofauti”,Alisema Edward Charles Mkazi wa Kahama mjini.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu umegundua kuwa kuna baadhi ya Vifaa ambavyo havipo katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na vipimo mbalimbali vya mifupa hali ambayo mwananchi anapoenda kutafuta huduma za vipimo huambiwa kuwa aende katika baadhi ya zahanati zilizopo jirani kwa ajili ya kupatiwa huduma hizo huku wakitumiagharama kubwa kupata vipimo hivyo.

Katika Hospitali ya Halmashuri ya Mji wa Kahama kuna baadhi ya Watumishi ambao wana maduka ya Dawa yaliopo jirani na Hospitali hiyo, hivyo hufanya kzi kwa muda mfupi huku muda mwingi wakiwa katika Maduka ya Dawa wakiendesha Biashara zao hali ambayo wagonjwa wengi hukosa huduma kwa Wakati na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa Wagonjwa.

Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya mji wa Kahama imekuwa ikitoa huduma za kiafya kwa Wananchi wengi kutoka Wilaya za Jirani ikiwemo zile za Nyang’wale , Bukombe na Mbogwe kutoka  Mkoani Geita, Wilaya ya Urambo,Kaliuwa pamoja na Nzega  Mkoani Tabora na hivyo kufanya tatizo la upungu wa Dawa katika Hospitali hiyo kuwa changamoto kubwa kwa Wagonjwa kupata huduma kwa wakati muafaka.

No comments:

Powered by Blogger.