LIVE STREAM ADS

Header Ads

MASHINDANO YA RIADHA YA ROCK CITY MARATHON 2015 YANAFANYIKA HII LEO JIJINI MWANZA.

Adella Lamsa ambae ni Mratibu wa Mashindano ya Riadha ya Rock City Marathon 2015 kutoka Kampuni ya Capital Plus International akizungumza katika uzinduzi wa Usaili wa mashindano hayo uliofanyika hivi karibuni Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mashindano hayo yanafanyika hii leo Jijini Mwanza na fainali zake zitakuwa katika Uwanja wa CCM Kirumba hivyo wananchi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kushuhudiwa wakimbiza upepo kutoka Tanzania na Mataifa jirani wanavyomenyana kwa ushindani mkali.

Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International na kudhaminiwa na Makampuni mbalimbali ikiwemo Mdhamini Mkuu Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF, Precision Air, Bodi ya Utalii Tanzania, New Mwanza Hotel na Bank M ambapo lengo lake ni kukuza mchezo wa riadha pamoja na kuhimiza utalii wa ndani.
Kuona Uzinduzi BONYEZA HAPA na Kuona Usaili  BONYEZA HAPA

No comments:

Powered by Blogger.