LIVE STREAM ADS

Header Ads

MZEE WA MIAKA 62 APANIA MBIO ZA ROCK CITY MARATHON 2015 ZINAZOTAJARIA KUFANYIKA JIJINI MWANZA.

Mzee Manumbu Buseni mwenye Umri wa Miaka 62 (Pichani) Mkazi wa Jijini Mwanza jana alijiandikisha kushiriki Mashindano ya mbio za Rock City Marathon 2015 yanayotarajia kufanyika jumapili Novemba 15,2015 yakipita katika viunga mbalimbali vya Jiji la Mwanza na kuhitimishiwa katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mzee Buseni alichukua fomu ya kushiriki mbio za kilomita 21 na hivyo kuungana na washiriki wengine 63 wakijumuisha mbio za kilomita mbalimbali waliojiandikishia katika kituo cha Nyamagana ambao tayari wamekwisha chukua fomu za ushiriki wa mbio hizo ambazo huandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International.

Alisema kuwa ameamua kushiriki mashindano hayo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha vijana kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo riadha pamoja na kujiimarisha zaidi kiafya kwa kuwa riadha ni mazoezi bora ya viungo huku akiendeleza matarajio yake makubwa ya kuibuka na ushindi katika mashindano hayo. 
Mshiriki mwingine Maryday Nyamugwa Nyangeresi (40) nae aliwahimiza wapenzi wa riadha kushiriki mbio hizo ambapo kesho ni siku ya mwisho ya usaili.
Nae Pascal Odiro ambae ni wakala wa uandikishaji katika Uwanja wa Nyamagana alisema kuwa zoezi la uandikishaji linaendelea vyema japo amekutana na changamoto ya baadhi ya wananchi kuhofia kushiriki mashindano hayo ya Rock City Marathon 2015 kutokana na kuhofia washiriki kutoka nchi jirani ya Kenya ambao katika mashinda ya miaka iliyopita wamekuwa wakiibuka kidedea.
Rock City Marathon 2015 ni Jumapili Novemba 15 Jijini Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.