LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAMLAKA YA MAPATO MKOANI KAGERA YAFANIKIWA KUVUKA LENGO LAKE YA UKUSANYAJI WA KODI.

Na:Elisa Anatory, Kagera
Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani Kagera imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 12.7 ikiwa ni kodi za ndani na ushuru wa forodha katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Octoba mwaka huu.

Akizungumza juzi katika kikao cha tathmini ya ukusanyaji wa Mapato Mkoani Kagera, Meneja wa Mamlaka hiyo Mkoani humo Mbaluku Abii, alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2015/16, lengo la Mamlaka hiyo lilikuwa ni kukusanya kiasi cha shilingi Bilingi 5.67 hivyo Mamlaka imefanikiwa kuvuka lengo ililojiwekea.

Pamoja na mafanikio hayo, Abii alibainisha kuwa bado Mamlaka hiyo inakabiriwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kulipa kodi kwa wakati huku wengine wakikwepa kutumia mashine za kutolea risiti za kielekroniki za EFD's.

No comments:

Powered by Blogger.