LIVE STREAM ADS

Header Ads

NSSF KAHAMA YAFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI SITA KWA MWEZI MJINI KAHAMA.

Na:Shaban Njia,Kahama
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Kahama (Wilaya ya Kahama kupitia NSSF ina hadhi ya Kimkoa) kupitia Wanachama wake walio katika sekta Rasmi na isiyo rasmi umeweza kufanikisha kukusanya  kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kwa kila mwezi kutoka kwa Wanachama wake waliojiunga na mfuko huo Wilayani hapa.

Akizungumza na wandishi wa habari jana, Meneja NSSF Mkoa wa Kahama Omary Mziya alisema kupitia wanachama walio katika sekta rasmi, Shirika limeweza kukusanya kiasi cha shilingi  bilioni 2.8 huku walio katika sekta isiyo rasmi wakisaidia kusanyaji wa kiasi cha shilingi billion 1.8.

Alisema kuwa moja ya vitu vinawavutia wanachama wengi kujiunga na NSSF ni pamoja na fao la Matibabu ambalo linaonekana kuwa mhimu na hivyo kuwapa kipaumbele katika kujiunga na mfuko huo wa Hifadhi ya jamii hapa nchini kwa kutoa elimu .

“Tunatoa elimu kwa Wananchi juu ya kujiunga na Mfuko huo pamoja na faida zake  popote tunapotembelea ikiwa ni sambamba na kuyanadi  mafao yote nane tunayoyatoa kwa Wanachama wetu hali ambayo inatoa hamasa kwa vikundi mbalimbali kujiunga na hivyo kufanikisha kupata wanachama wengi”.  Alisema Mziya.

Meneja huyo aliendelea kusema kuwa moja ya mafanikio ya shirika hilo ni pamoja na kupata wanachama wengi kutoka katika migodi miwili ya Dhahabnu iliyopo katika Wilaya ya Kahama ambayo ni ile ya Buzwagi na Bulyanhulu ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa na Wafanyakazi wengi ambao wamejiunga na mfuko huo.

Hata hivyo Mziya alisema kuwa kwa sasa Shirika lake limehamishia nguvu zake katika makundi ya mama lishe pamoja na Bodaboda ili kuhakikisha kuwa makundi hiyo yanaingia kujiunga na NSSF ili kuwawezesha kuweka akiba ambayo itaweza kuwasadia katika maisha yao ya baadaye.

“Tumefanikiwa kwa kiasi Fulani kuweza kuwashawishi kundi la waendesha pikipiki (Bodaboda) pamoja na mama lishe kujiunga na mfuko huu kwani utawasaidia hapo baadaye na hali siyo mbaya kwani wameonyesha mwitikio mkubwa na hasa wanaposikia kuna mafao ya matibabu ya watu wanne tegemezi katika familia”. Aliongeza Mziya.

Aidha alisema kuwa kila mwaka NSSF inatoa Elimu kwa bodaboda katika kuhakikisha kuwa ajali za barabarani zisizokuwa za lazima zinapungua pamoja na kuwa na nguvu kwa ajili ya kuendesha pikipiki hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa kundi hilo.

Meneja huyo aliwataka Wananchi kuunda vikundi mbambali vya ujasiliamali hali ambayo inaweza kuwasadia kupata hata mikopo kupitia mfuko huo wa Hifadhi ya jamii pamoja na makundi mbalimbali ya ujasiliamali na kuongeza kuwa kwa sasa wameamua kuingia katika makundi ya watu wenye kipato cha chini ambao wapo katika sekta isiyo rasmi.

“Kwa sasa hapa nchini kundi la watu walio katika sekta isiyo rasmi ni kubwa tofauti na lile lililopo katika sekta rasmi ndio maana tumeamua kuelekeza nguvu kubwa katika kundi hilo ili waweze kujiunga na mfuko huu na hasa kwa ajili ya kupata fao la matibabu ambalo ndio muhimu katika jamii kubwa iliyopo hapa nchini”, Alisisitiza Mziya.

No comments:

Powered by Blogger.