LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAHANGA WA MGODI WA NYANGARATA WAOMBA KUHAMISHIWA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO

Na:Shaban Njia
WAHANGA waliofukiwa na kifusi na kukaa siku 41 ndani ya shimo katika Mgodi wa Nyangarata Kahama Mkoani Shinyanga wameiomba Serikali iangalie uwezakano wa kuwahamishia katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza ili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kauli hiyo ilitolewa na Wahanga hao baada ya kutembelewa jana na Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Edward   Lowassa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama walipolazwa kwa matibabu zaidi pamoja na kuangaliwa Afya zao.

Akiongea kwa taabu mbele ya Waziri Mkuu huyo Mstaafu mmoja wa Wahanga hao Chacha Wambura alisema kuwa kwa sasa hali ya afya zao sio nzuri na kuongeza kuwa ni bora wakaamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando ili waweze kupatiwa matibabu zaidi.

Kwa upande wake Mhanga mwinge Joseph Burule alisema kuwa pia kuondokewa na Mwenzao Onyiwa Kaiwao pia kuewatia haofu ya kuendelea kushi hali ambayo kwa kubadilisha mazingira katika Hospitali hiyo kunaweza kuwaondolea mawazo

“Kuhusu kifo cha mwenzetu  Onyiwa Kaiwao kimetupa hofu kubwa na tulipatwa na msituko hivyo jana mgetuuliza  kuhusiana na hilo huenda tungezimia kwani tuliishi shimoni kwa siku 41 na kuokolewa wote tukiwa hai,tukipewa chakula tulikuwa tukila kwa pamoja huku tunataniana kwamba vipi kule”,alisema Burule.

Aidha Burule alimweleza Lowassa kuwa kitendo cha kuwatembelea hospitalini hapo kimewapa faraja kubwa  na kuwapa moyo kwa kuwa yeye ni kiongozi Mkubwa hapa nchini hivyo itaweza kuwatia moyo na Viongozi wengine kuja katika Hospitali kwa nia ya kuwapa pole.

Waziri Mkuu huyo alisema kuwa fedha alizowapatia Wahanga hao zitawasaidia katika mambo madogomadogo pamoja na kujikimu kwa muda wataoendelea kutibiwa hospitalini hapo huku wakisubiri afya zao zikapoimarika ili waweze kurudi majumbani na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa..

“Kwa kweli tumpongeze Lowassa kwani ni kiongozi anayetakiwa kuigwa kwani tangu tumeletwa hapa hakuna kiongozi wa serikali wa ngazi za juu aliyefika hapa kutujulia hali, tunaishi kwa kumuomba mungu kwani alipofariki mwenzetu na ukilinganisha alikuwa hali nzuri  na sisi huenda hali zikabadirika”,aliongeza burule.

Kwa upande wake Lowassa alisema kuwa amefika katika hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa lengo la kuwapa salama pole huku akiwapatia shilingi 500,000 kwa kila mmoja huku akiwaahidi kufikisha salamu hizo kwa viongozi wengine wa ngazi za juu  ili nao wafike hapo kuwaona na kutoa misaada walionao.

Nae Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga CHADEMA Salome Makamba akiwatuliza wananchi waliokuwa wakimshangilia Lowassa kwa kumuita Rais aliwataka wasifanye fujoa mkatika mazingira ya Hospitalini bali wasubili Lowassa atoke katika mazingira hayo ili azungumze nao.

“Ninawasihi msiwapigie kelele wagonjwa tumsubili Lowassa atokea nje ya eneo la hospitali tafadharini sana mtazungumza naye tu hapa amekuja kuwapa pole wagonjwa hajaja kwa lengo la siasa atawasalimia tu”. Aalisema Makamba.

No comments:

Powered by Blogger.